Utunzaji wa maji safi na salama hutolewa hasa na Mamlaka ya Maj i Mwanza (MWAUWASA) ambayo sasa ni 92% kwa watu wote wanaoishi katikati Jiji na 67% kwa watu wanaoishi katika maeneo ya pembezoni.
Kwa sasa Jiji la Mwanza limekamilisha mradi mkubwa wa maji ambao unakadiriwa kuwaokoa watu 6,000. Hii itafikisha asilimia 73%. ya watu wanaopata maji Pia tuna mradi mpya wa maji katika eneo la Lwanhima ambalo baada ya kukamilika utagarimu Tsh 2,218,000,000.00 (WSDP)
Sekta ya maji ina lengo la a kufikisha huduma ya maji katika maeneo yote ya pembezoni mwa mji hususani katika maeneo ya Kata za Kishiri, Lwanhima na Luchelele pia kuhakikisha kuwa maeneo yote ya utoaji huduma za kijamii kama Zahanati, Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya, Shule za Msingi na Shule za Sekondari zinapata huduma za Maji endelevu.
Mpaka sasa Idara imefikisha huduma ya maji katika maeneo ya Fumagila, Luchelele ziwani na Kilimo kishili kupitia Mfuko wa Maji vijijini na pia inaendelea na ujenzi wa mradi wa usambazaji maji katika kata ya Lwanhima.
Aidha, katika sekta hii inatoa elimu ya usimamizi wa miradi ya maji kwa vikundi vya watumiaji wa maji (COWSO) na wasimamizi wa magati ya maji pale mradi unapokamilika.
Hata hivyo huduma ya maji safi na salama kwa baadhi ya taasisi za serikali imekamilika, mpaka sasa shule za msingi zenye huduma ya maji ni 70, shule za sekondari zenye huduma ya maji ni 27, zahanati zenye huduma ya maji ni 12 na vituo vya afya vyenye huduma ya maji ni 2.
Huduma ya Maji safi na Salama katika maeneo ya pembezoni mwa mji imeongezeka kutoka asilimia 42 mwaka 2010 hadi kufikia asilimia 62 mwaka 2018 na tumefanikiwa kuongeza idadi ya vituo vya kuchotea maji kutoka 29 hadi 82 kwa maeneo ya Luchelele ziwani, Kishili kilimo na Fumagila kwa jumla ya miradi ya maji iliyokamilika.
Naomba kuwasilisha,
Eng Zubeda Saidi
K N Y. MKURUGENZI WA JIJI
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.