MAFANIKIO YALIYOPATIKANA IDARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII 2016/2017
Utangulizi
Halmashauri ya jiji la Mwanza ina jumla ya vituo 75 vya kutolea huduma za Afya. Pia ndani ya Wilaya kuna Hospitali ya Mkoa Sekoutoure na Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Clinic zinazojitegemea, na vituo vinavyotoa huduma ya uzazi (PRINMAT) Mchanganuo wa vituo vya kutolea huduma za Afya ni kama ifuatavyo:
Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2015/2016 ni pamoja na
2. Utoaji wa huduma za Chanjo kwa watoto na wajawazito
Idara imepokea dawa za chanjo zifuatazo toka Mkoani kwa kipindi cha 2015 hadi 2016 Chanjo ya BC,chanjo ya Penta valent dozi, Chanjo ya Surua/Rubella, Chanjo ya bOpv Chanjo ya Pepopunda dozi (TTv), Chanjo ya PCv13,Chanjo ya Rotarix, Mabomba ya sindano 0.05ml, Mabomba ya sindano 0.5ml, Makasha maalumu ya (safety boxes)
Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za chanjo kutoka vituo 30 kwa mwaka 2015 hadi vituo 35 kwa mwaka 2016. Pia Kuendelea kuimarisha utoaji wa chanjo kutoka aslimia 100 kwa mwaka 2015 hadi asilimia 106 kwa 2016 kwa chanjo ya Penta valent 3.
Kuendelea kutoa huduma ya chanjo ya mkoba kwenye maeneo yasiyo na huduma za chanjo karibu, vituo vya Mahina, Igoma, Sahwa, Mkolani na Nyegezi Fumagila na Shadi.
3. UPATIKANAJI NA USAMBAZAJI WA MADAWA NA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI, VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI 2015/2016
Dawa muhimu (tracer medicines) zilipatikana kwa kiwango cha asilimia themanini na moja (85 %) katika vituo vya kutolea huduma za afya (15) Hospitali 1, vituo vya afya 2 na zahanati 12.vinavyomilikiwa na Halmashauri. Pia vituo vyote vilipata mgawo wa dawa za serikali kutoka MSD na kusambazwa.
Upatikanaji wa damu salama ni jumla ya lita 853 za mls 450 zilizopatikana ambayo ni sawa na asilimia 25% kati ya malengo ya lita 3400 kwa miezi 8.
Udhibiti wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa watoto wa shule za msingi wenye umri wa miaka 5 hadi 15 ambapo walengwa walikuwa 88,323 kati ya hao wanafunzi wa kike ni 45,267 wanafunziwa kiume ni 42,362. Jumla walIopata dawa za minyoo ya tumbo ni 86,237 ni sawa na asilimia 91.6 na walioata dawa za kichocho ni 86,127 sawa na aslimia 91.5%
4. UDHIBITI WA MAGONJWA YA MALARIA PAMOJA NA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA
Wagonjwa waliopimwa malaria 47,138, waliopimwa kwa kutumia mRDT ni 11,767 na BS 35371 Mama wajawazito walipimwa malaria 4911 kati yao 345 waligundulka na malaria Jumla ya akinamama wajawazito 9668 walipewa dawa za SP kukinga watoto walioko tumboni dhidi ya Malaria ,akinamama wajawazito 1142 pamaoja na watoto 844 walipewa vyandarua vyenye viuatilivfu vya muda mrefu kwa ajili ya kujikinga na malaria.
5. UHAMASISHAJI WA JAMII KUJIUNGA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF/TIKKA
6. UDHIBITI WA UGONJWA WA UKIMWI.
Kwa mwaka 2015/2016 mpango wa upimaji wa hiari umefanyika na kupima watu 49,086 kati ya hao wanaume ni 21,803,na wanawake27,283, kati ya hao walioonekana na maabukizi ni 3,973 wakike 2478 na wakiume 1,495
Kwa kupitia upimaji unaoanzishwa na mtoa huduma wamepimwa watu 3,3215 kati yao 14681 ni wanaume na 18534 ni wanawake, waliopata maabukizi ni 2357 na kati yao 897 wanaume na 1460 wakike.
7. USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA USTAWI WA JAMII
Tumetengeneza vitambulisho vya wazee 5872 na kugawiwa ,Mashauri 239 yaliendeshwa kwa wanandoa wenye migogoro katika familia zao, watoto kesi 213 zimetolewa hukumu na kesi 26 bado zinaendelea , wazazi waliokuwa hawatoi matunzo wamewapatia watoto 246 wao matunzo yenye thamani ya Tsh 18,593,450 kwa njia ya kuandikishana ofisini ,Jumla ya watoto wa wanaoishi mitaani 1314 walifahamika ,watoto 179 wameondolewa na kuunganishwa na familia zao, Jumla ya kesi za watoto zipatazo 239 zimesikilizwa mahakamani kati ya hizo, jumla ya kesi 37 za watoto zilifunguliwa , kati ya hizo kesi 27 za ubakaji wa watoto, zilihukumia, kesi 6 watoto walifanya makosa, kesi 4 watoto kupewa ujauzito.
8. USIMAMIZI WA USAFI WA MAZINGIRA
Kiwango cha kaya zenye vyoo bora kimeongezeka toka 49% hadi 53% hii imetokana na kufanyika kwa kampeni ya usafi wa mazingira katika kata za Buhongwa, Lwanhima,Mkolani,Nyegezi,Luchelele,abatini,Igoma ,na Kishili.
Uhamasishaji wa jamii ulifanyika katika masuala yafuatayo -unawaji wa mikono mara kwa mara baada ya kutoka chooni,Katika maeneo yanayouza vyakula kama vile Hotel,Migahawa,na mama lishe /Baba lishe wateja kunawa mikono kwa maji safi na sabuni
Kutoa elimu ya afya kwa jamii katika kata zote 18 na mitaa 175 na pia kudhibiti milipuko ya magojwa ya kuambukizwa .
MIKAKATI YA IDARA
Idara imeanza kujenga jengo litakalotumika kama wodi ya wanaume katika Hospitali ya Nyamagana.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.