Watumishi wastaafu wametakiwa kutumia kiinua mgongo kwa matumizi ambayo ni sahihi, rai hiyo imetolewa mapema leo Januari 29, 2026 na Afisa Utumishi Mkuu wa Jiji la Mwanza Ndg. Musa Mbyana ambaye pia amemuwakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
" Niwasihi mliopata kiinua Mgongo kuendelea kutumia kwa matumizi ambayo ni sahihi, kama ulikua haujanunua gari, haujajenga, kiinua mgongo siyo kwa matumizi ya kununua hivyo vitu" amesisitiza Ndg. Mbyana
Mbyana pia ameendelea kwa kuwaasa wastaafu kujali afya zao kwa kufanya mazoezi huku akiishukuru Idara ya Elimu kwa kuwezesha hili
" Niwashukuru Idara ya Elimu kwa kutupa mwamko na tukijaaliwa tutafanya hivyo kwa wastaafu wote, Ninyi ni walimu na kweli mmetufundisha, niwashukuru kwa elimu hii mliotupa".
Kwa upande wao wastaafu wameshukuru na kuomba jambo hili liwe endelevu lisiishie kwao tu.
Hafla hii imejumuisha wastaafu 23 waliostaafu kwa kipindi cha Mwaka 2025 kutoka Idara ya Elimu Msingi na Elimu Sekondari.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.