Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 23, 2026 amezindua rasmi meli mpya ya kisasa ya MV NEW MWANZA katika Bandari ya Mwanza Kusini, iliyojengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 120.56.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Waziri Mkuu amesema ujenzi wa meli hiyo ni ushahidi wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha usafiri wa majini katika Ziwa Victoria ili kurahisisha huduma za usafiri na biashara kwa wananchi.
Ametoa maelekezo kwa Wizara ya Uchukuzi kuendeleza ujuzi uliotumika katika ujenzi wa meli hiyo, huku akiagiza TASHICO kushirikiana na wadau kuhakikisha mradi unalindwa kwa bima, kuzingatia ushauri wa kitaalamu na kudumisha mahusiano mema ya kikanda.
Aidha, amezitaka wizara zinazosimamia miradi ya maendeleo kufanya tathmini ya miradi iliyosimama kutokana na ukosefu wa malipo kwa wakandarasi ili fedha zipatikane na miradi ikamilike kwa manufaa ya jamii.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.