Kuratibu shughuli zote zihusuzo uchaguzi (uchaguzi wa serikali za mitaa, uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo zote zitakazo jitokeza baada ya uchaguzi kufanyika).
Kuratibu mazoezi yote ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa uchaguzi mkuu na Orodha ya wapiga kura kwa Uchaguzi wa serikali za mitaa
Kuratibu maswala yote muhim kwa ajili ya kuwezesha mazoez ya uchaguzi (maswala hayo ni pamoja na maandaliz ya uteuz wa wagombea, kuratibu kampeni za wagombea, maadaliz ya vituo vya kupigia kura, mafunzo kwa washiriki wote wa mazez ya uchaguzi. Mambo yote haya yanafanyika kwa ushiriji wa karibu na TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI na Wizara inayosimamia Uchaguzi wa serikali za Mitaa).
Kushirikiana na Idara ya Utumishi kuhakikisha mafunzo ya mara kwa mara yanafanyika kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa Mujibu wa Sheria
Kumshauri Mkurugenzi juu ya maswala yote yahusuyo uchaguzi katika Halmashauri ili kuwezesha mazoezi hayo kufanyika kwa mujibu wa Sheria
Kutekeleza majukumu mengineyo kwa maelekezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri