Ikiwa zimebaki siku Chache shule za Msingi na sekondari kufunguliwa mapema januari 13,2026 ili kuanza muhula mpya wa masomo 2026 Wilaya ya Nyamagana imeendelea kuboresha mazingira rafiki kwa ajili ya Wanafunzi kujisomea.
Ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba akiwa ameambatana na menejiment amefanya ziara Leo Januari 7,2026 na kukagua miradi ya kimkakati katika Wilaya ya Nyamagana.
Katika ziara hiyo amekagua miundombinu ya Afya na ya shule za Msingi na Sekondari huku akitoa ahadi ya madawati kwa baadhi ya shule zinazoonekana kuwa na adha kubwa ya ukosefu wa madawati nakuongeza kasi ya ujenzi wa madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani.
“Hakikisheni mnajua kila darasa wanakaa wanafunzi wangapi na pungufu ya madawati ni mangapi? Tupate Idadi kamili madawati yaletwe” amesema Wakili Kibamba
Vilevile Mkurugenzi amekagua karakana ya utengenezaji wa madawati eneo la Buhongwa ambapo amejilidhisha kwa kuona madawati takribani 3000 yamekwisha tengenezwa kwa kiwango bora huku mengine yakiendelea Kutengenezwa.
Mbali na hayo pia Mkurugenzi amehitimisha kwa kukagua ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi wa Jiji kwa muundo wa Ghorofa linalogharimu kiasi cha shilingi 491,111,988 na kutoa maelekezo kwa injinia kuhakikisha anasimamia na linaisha kwa wakati uliyopangwa.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.