HUDUMA TUNAZOTOA
1 Kuwajengea uwezo wafugaji juu ya ufugaji bora,
2. Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Samaki kwenye kata husika,
3. Kusimamia kanuni za ufugaji bora ili kuhakikisha kuwa wafugaji wanazalisha kwa tija ukilinganisha na mifugo na maeneo waliyonayo.
4. Ukusanyaji wa mapato yatokanayo Machinjio na Vyanzo vingine vya mapato idara ya Mifugo na Uvuvi.
5. Kuboresha Mifugo,Samaki na mazao yake kwenye maeneo husika,
6. Kutoa elimu ya ugani kwa wafugaji wa Mifugo na samaki,
7. Kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora unakuwepo katika ngazi ya kaya,
8. Kuboresha miundo mbinu ya Mifugo na Uvuvi kwenye Kata husika,
9. Kusimamia sheria na kanuni za Mifugo na Uvuvi.
Taratibu za kupata huduma
Idara inao watumishi katika ngazi mbili katika utoaji wa huduma kama ifutavyo:-
i. Ngazi ya kata ( maafisa ugani kata)
ii. Ngazi ya makao makuu ( Mkuu wa Idara na wakuu wa vitengo)
Ngazi ya kata
Katika utoaji wa huduma kwa wadau wa Mifugo na Uvuvi ambao ni wafugaji,Maafisa ugani wana madaftari ya wafugaji katika maeneo yao ya kazi. Aidha wataalamu wana ratiba zao za kazi ambao ni utaratibu wa kazi zao za kila siku. Ratiba hizo huwezesha kuwatembelea wafugaji wao hususani Majumbani na mashambani kwa ajili ya kutoa huduma za ugani. Muda huo hutoa maelekezo , ushauri, pia kusimamia kanuni za ufugaji bora kulingana na mifugo wanayonayo.
Ngazi ya makao makuu
Huduma inayotolewa na wataalamu walioko makao makuu ni masuala ya utawala. Sambamba na hilo kupokea na kutatua masuala ya utaalamu kuhusiana na Mifugo na uvuvi, yanapokuwa yamekosa ufumbuzi yanapelekwa kwenye vituo vya utafiti ili kuhakikisha kwa shughuli za Mifugo na Uvuvi. zinaendelea bila kukwama.Pindi tu utatuzi au majibu yanapopatikana yanapelekwa kwa wataalamu ngazi ya kata ili yafikishwe kwa wafugaji ili wafanikishe shughuli zao.
Shughuli zote hizi zinafanyika chini ya mkuu wa Idara ambaye ndie mwenye kuratibu mambo yote na mambo mengine yanayohusu Mifugo na uvuvi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.