Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Januari 23, 2026 ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa kituo cha kusukuma maji na matenki ya kuhifadhia maji katika mtaa wa Sahwa, Kata ya Lwanhima, Jijini Mwanza.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Waziri Mkuu amewataka wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, akisisitiza kuwa Serikali itasimamia utekelezaji wake kwa ukaribu ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi.
Ameelekeza pia Wizara ya Maji kuhakikisha fedha za miradi ya maji zinawasilishwa kwa wakati, akibainisha kuwa maji ni huduma muhimu ya kijamii isiyo na mbadala.
Kwa upande wake, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (MB), amesema Wizara yake kwa kushirikiana na MWAUWASA itaendelea kumsimamia mkandarasi ili mradi ukamilike kwa mujibu wa mkataba.
Mradi huo unaotekelezwa chini ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira ya Ziwa Victoria (LVWATSAN) unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi 450,000 wa Jiji la Mwanza pamoja na Wilaya za Magu na Misungwi, na utakapokamilika utachangia kuboresha upatikanaji wa majisafi na kupunguza magonjwa yatokanayo na maji machafu. Gharama za mradi ni zaidi ya Shilingi bilioni 46 na unatarajiwa kukamilika Desemba, 2026.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.