Mganga Mkuu wa Hospitari ya Wilaya ya Nyamagana katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza Dr. Pima Sebastian Pima, leo Julai 24,2024 amezungumza na waandishi wa habari katika Ofisi yake iliyopo Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, kwa lengo la kuujulisha Umma juu ya huduma itakayotolewa tarehe 26 hadi 28 Julai, 2024 ya upimaji na uchunguzi wa awali wa Saratani ya Matiti.
Akizungumzia upimaji huo uliodhaminiwa na wizara ya Afya na Asasi ya JHPIEGO, Dr. Pima amesema kuwa zoezi la upimaji na uchunguzi huo litafanyika kwa Wanawake na Wanaume katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Sekou toure) na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, huku akisisitiza watu kujitokeza kupima bila kujali jinsia kwani kati ya Wanaume 10 imegundulika kuwa wanaume wanne(4) hukutwa na saratani.
Dr Pima amehitimisha kwa kusema "Ninatoa wito kwa Umma kuja kupima saratani kwani vipimo ni bure na ukigundulika unalo tatizo hilo utapata matibabu kwa haraka na hivyo kunusuru uhai wako na afya yako kabla tatizo halijafika hatua mbaya."
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.