Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amefanya ziara ya kukagua na kuzindua miradi ya elimu na afya katika Jiji la Mwanza.
Akiwa Sekondari ya Kisoko, ameagiza fidia ya Sh milioni 163 iliyobaki kulipwa haraka ili kupisha ujenzi wa mabweni, huku akiishukuru Serikali kwa kutoa zaidi ya Sh milioni 584 kupitia SEQUIP.
Katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana, amemtaka mkandarasi wa jengo la ghorofa tano kuongeza kasi ya ujenzi, akisisitiza mradi wa zaidi ya Sh bilioni 2 ukamilike kwa wakati ili kuanza kutoa huduma muhimu ikiwemo ICU, dharura na upasuaji.
Aidha, amezindua Shule ya Msingi Kanyerere iliyogharimu zaidi ya Sh milioni 424 na kupongeza ushirikiano wa Serikali, wananchi na wadau.
Ziara hiyo imeonesha dhamira ya Serikali kuimarisha huduma za elimu, afya na miundombinu kwa wananchi wa Mwanza.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.