Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, Februari 12, 2026 ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Msingi ya Amali iliyopo Kata ya Kishiri, Jijini Mwanza.
Baada ya kukagua mradi huo, ameagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya wiki tatu kama ilivyopangwa.
Amesema kukamilika kwa shule hiyo kwa wakati kutawawezesha wanafunzi kuanza masomo katika mazingira bora na rafiki kwa maendeleo yao ya kitaaluma na kijamii.
“Muda uliopangwa uzingatiwe. Shule ianze kufanya kazi mara tu baada ya kukamilika,” amesisitiza.
Katika hafla hiyo, RC Mtanda pia ameipongeza Shule ya Sekondari Igoma kwa kuongoza kiwilaya katika matokeo ya Kidato cha Nne 2025 Wilaya ya Nyamagana.
Akisoma taarifa ya mradi, Mwalimu Mkuu wa Sekondari Igoma, Anthony Masanja, amesema shule ilipokea Shilingi 330,700,000 kupitia Mradi wa BOOST tarehe 1 Julai 2025.
Ameeleza kuwa hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 75, ambapo Shilingi 258,600,000 zimetumika na Shilingi 72,100,000 zimesalia kukamilisha kazi zilizobaki.
Mradi unasimamiwa na Ofisi ya Mhandisi wa Jiji la Mwanza, huku mkandarasi akiwa Ndugu Eliawony Makundi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.