• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

MKUU WA MKOA AIPONGEZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KWA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UHABA WA MADAWATI

Posted on: February 12th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika kupunguza kwa kiwango kikubwa changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za elimu ya awali na msingi.

Pongezi hizo amezitoa wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 2,939 kwa shule 13 zilizopo ndani ya Jiji la Mwanza. Madawati hayo yametengenezwa kwa gharama ya Shilingi 440,800,000 ikiwa ni sehemu ya awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango wa kuimarisha miundombinu ya elimu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza bado unakabiliwa na upungufu wa madawati 61,808, huku Jiji la Mwanza likiwa miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi. Hata hivyo, amepongeza hatua ya uongozi wa Jiji kuanzisha mkakati mahsusi wa kukabiliana na hali hiyo.

Ameeleza kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza kutapunguza kwa kiasi kikubwa uhaba huo na kubakiza takribani madawati 2,000 pekee, ambayo yamepangwa kushughulikiwa ndani ya mwaka huu wa fedha.

“Ninawapongeza kwa kasi hii ya utekelezaji. Ni wajibu wa kila halmashauri kuhakikisha mwanafunzi anapata mazingira bora ya kujifunzia,” amesisitiza.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amezitaka halmashauri zenye changamoto kubwa ya madawati, ikiwemo Jiji la Mwanza, Kwimba, Magu na Sengerema, kuanzisha karakana za kutengeneza madawati ili kupunguza gharama na kuongeza uzalishaji.

Ameongeza kuwa ofisi yake itafanya ufuatiliaji wa karibu ndani ya miezi mitatu ijayo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kibamba, amesema lengo lao ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini darasani.

Amebainisha kuwa mgawanyo wa madawati umezingatia mahitaji halisi ya kila shule, na kwamba ifikapo Juni mwaka huu kila darasa litakuwa na wastani wa madawati 30 ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA UCHAGUZI October 19, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA SEMINA JIMBO LA NYAMAGANA October 21, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 29, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 09, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MTANDA AFANYA ZIARA YA MIRADI MWANZA, ASISITIZA KASI NA UWAZI WA UTEKELEZAJI

    February 12, 2026
  • MKUU WA MKOA AIPONGEZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KWA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UHABA WA MADAWATI

    February 12, 2026
  • RC MTANDA ASISITIZA UKAMILISHAJI WA SHULE YA AMALI KISHIRI NDANI YA WIKI TATU

    February 12, 2026
  • KATIBU TAWALA NYAMAGANA AWAHIMIZA WADAU WA BIASHARA KUSHIRIKIANA KUKUZA UCHUMI

    February 11, 2026
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.