Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe waliyochaguliwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mujibu wa sheria katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza waapishwa leo Novemba 29,2024 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Nganza, tayari kwa kuanza kutekeleza majukum yao.
Wenyeviti wa Mitaa 175 na wajumbe 1050 wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Jimbo la Nyamagana waliochaguliwa kwa kura za ndio mnamo Novemba 27,2024 wamekula kiapo cha haki na utii mbele ya Hakimu Mkazi Nyamisango M. Bulemo.
Hakimu Bulemo Amewasisitiza wenyeviti na wajumbe kuwa wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia kiapo hicho kwa kuwa waadilifu kwa wananchi wanaowahudumia kwa kujishusha na siyo kujikweza na kuwaelekeza atakayeenda kinyume na kiapo alichoapa atachukuliwa hatua za kisheria.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg.Peter Lehhet, amewapongeza Wenyeviti na Wajumbe kwa ushindi mnono waliyoupata na kuwataka watekeleze majukumu yao kwa wananchi kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Nchi zinavyoelekeza.
Ikumbukwe uchaguzi wa wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa hufanyika kila baada ya miaka minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu, ambapo ķwa Tanzania unatarajiwa kufanyika 2025.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.