Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe, Omary Mohamed Mchengerwa amehudhuria hafla ya Utiaji Saini Ujenzi wa soko la Samaki Mkuyuni akiwa kama mgeni rasmi leo Oktoba 16, 2024 katika Uwanja wa Furahisha Manispaa ya Ilemela.
Mhe, Mchengerwa amesema mradi huu ni moja kati ya miradi inayotekelezwa kupitia Miradi ya uboreshaji Miji Tanzania (TACTIC) huku akimshukuru Rais Mhe Dkt, Samia Suluhu Hassani kwa kutoa Fedha nyingi katika Miradi ya maendeleo na kukiri kuwa huu ni utekelezaji wa Irani ya Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili, Kiomoni K. Kibamba na Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe, Sima C.Sima wametia saini mkataba wa makubaliano ya Ujenzi wa Soko la Samaki Mkuyuni ambalo litagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 7.364 ambapo mradi huu utatekelezwa kupitia miradi ya uboreshaji Miji Tanzania (TACTIC)
Naye Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe, Stanslaus Mabula ameishukuru serikali kwa niaba ya Wananchi na kusema Ujenzi wa Soko ukikamilika utawasaidia wafanyabiashara wa Samaki takribani 800 kukuza vipato vyao na kupunguza msongamano katika Soko dogo la Mswahili.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.