Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI amefanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo ya Kimkakati inayotarajiwa kutekelezwa /na Mingine ipo kwenye utekelezaji na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ukarabati wa Mabweni shule ya sekondari Nganza,Eneo la ujenzi maegesho ya malori ya mizigo –Buhongwa,Ujenzi wa stendi ya Mabasi –Nyegezi ,Mradi wa Umeme wa Jua – Hospitali ya wilaya Nyamagana,Ujenzi wa Barabara ya mawe Mulungushi, Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa -Igoma na Ujenzi wa Madarasa Manne shule ya msingi Nyashana.
Miradi yote iliyotembelewa na Mheshimiwa Jaffo ipo kwenye hatua mbali mbali za utekelezaji , suala ambalo limemfurahisha Mheshimiwa Waziri kwa namna Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ,Mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Mkurugenzi wa Jiji na timu yake ya wataalamu wanavyotekeza miradi mikubwa kwa ufanisi mkubwa .
Akihitimisha ziara yake katika Shule ya Msingi Nyashana Mheshimiwa Jaffo amehaidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya kuanzisha shule nyingine kata ya mbugani kutokana na wingi wa wanafunzi katika shule ya msingi Nyashana. Aidha Mheshimiwa Jaffo amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa kujenga madarasa mengi na yenye viwango “nimesikia Mkurugenzi amejenga madarasa mazuri kama haya niliyoyaona 60 shule mbali mbali ndani ya Jiji! Nikupongeze binafsi kwa sababu nilishaagiza madarasa yote yanayojengwa sasa kuwekewa marumaru chini na wewe tayari ilikwishaanza kutekeleza Hongera sana” amesema Mheshimiwa Jaffo.
Mkurugenzi wa JIji la Mwanza ,Kiomoni Kibamba amesema kwamba Halmashauri ya Jiji la Mwanza imekusudia kutekeleza miradi mingi ya kimkakati na hiyo iliyotembelewa na Mheshimiwa waziri ni sehemu tu ya miradi yote.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.