• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

WATENDAJI WA KATA NA MITAA JIJINI MWANZA WAHIMIZWA UWAJIBIKAJI KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO

Posted on: December 30th, 2025

Watendaji wa kata 18 na mitaa 175 katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamehimizwa kuwajibika ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao, hususan kwenye ufuatiliaji na ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.

Rai hiyo imetolewa Desemba 29, 2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili Kiomoni Kibamba, wakati akizungumza na watendaji hao.

Ameeleza kuwa kila mtendaji anatakiwa kutimiza wajibu wake kwa nafasi aliyonayo ili kuhakikisha malengo ya halmashauri yanafikiwa.

Mkurugenzi  amesisitiza umuhimu wa ukusanyaji wa mapato akieleza kuwa kwa sasa mfumo wa Balozi System utaendelea kutumika, huku akibainisha kuwa ofisi rasmi za ukusanyaji wa mapato zitafunguliwa katika ngazi ya kata  na kila kata itakuwa na meneja maalum wa kuratibu masuala ya ukusanyaji wa mapato.

Katika kuhakikisha ufanisi unaongezeka, Wakili Kibamba amewataka watendaji kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu na kuzingatia malengo yaliyowekwa.

Ameagiza kila mtendaji wa mtaa kuhakikisha anatembelea biashara zisizopungua thelathini (30) kwa siku, ili kubaini na kusimamia ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali kwa wafanyabiashara wanaostahili kulipa..

Aidha, amebainisha kuwa watendaji wote watapimwa kwa utendaji wao wa kazi, hususan katika eneo la ukusanyaji wa mapato, na kuwataka kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila mwezi.

Kwa upande wake, Afisa Utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bw. Mussa Mbyana, amewataka watendaji hao kuzingatia na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa. Pia amesisitiza umuhimu wa kupanga ratiba zao vizuri ili waweze kuwahudumia wananchi ipasavyo katika maeneo yao ya kazi.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA UCHAGUZI October 19, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA SEMINA JIMBO LA NYAMAGANA October 21, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 29, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 09, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MBUNGE WA NYAMAGANA MH. JOHN NZILANYINGI ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATA YA MIRONGO

    January 09, 2026
  • MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA AKAGUA MIUNDOMBINU YA KIMKAKATI NYAMAGANA.

    January 07, 2026
  • MBUNGE WA NYAMAGANA AKUTANA NA MENEJIMENTI YA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA

    January 06, 2026
  • UZIO WAVUNJWA MAHINA, BARABARA YA UMMA YAFUNGULIWA.

    December 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.