Akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza hususani wa Wilaya ya Nyamagana Leo Disemba 5 , 2025 katika uwanja wa Nyamagana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ( Mb) amesema Tanzania inapaswa kuheshimu sekta binafsi kwani kupitia sekta binafsi ajira mbalimbali huzalishwa. Leo hii unaenda kuharibu sekta binafsi ajira za baadhi ya watu zitapatikana kweli?. Waziri Mkuu amesema.
"Hakuna serikali inayoweza kuajili wananchi wake wote serikalini, Watanzania yatupasa tuelewe umuhimu wa sekta binafsi kwani sekta hii ni muhimu sana nchini kwetu wapo vijana ambao wameajiliwa kupitia sekta binafsi lazima tuziheshimu na tuelewe umuhimu wake , wapo watu watoto wao wamesomeshwa kupitia sekta binafsi sababu ya ajira tuzilinde na sio kuziharibu"
Aidha katika Mkutano huo wa Hadhara ambao ulikuwa na Lengo la kueleza hali ya kiusalama nchini kwa Yale yaliyotokea Oktoba 29 Waziri Mkuu amesema Watanzania twapaswa kulinda amani na Utulivu wa nchi yetu kwani bila uwepo wa amani tatizo la umasikini ni ngumu kutatuliwa.
"Uwezi kupata kipato Cha Kutosha kama nchi yetu Haina Amani , huwezi kwenda kuzalisha kama nchi yetu Haina Amani watanzania yatupasa kulinda amani yetu"
Sanjari na hayo pia Waziri Mkuu ameelekeza Wizara ya ujenzi kuhakikisha mkandarasi anaesimamia daraja la mkuyuni linakamilika kwa wakati ili shughuli mbalimbali za huzalishaji ziweze kuendelea.
"Nimesikia hapa Kuna daraja linasuasua naomba nielekeze Wizara ya Ujenzi kuhakikisha daraja ili linakamilika kwa wakati nitakapo rudi kwa ziara ya kikazi nikute mambo yamekamilika"
Pia Waziri Mkuu amegusia suala la uadilifu kazini kwani kupitia udalifu uzembe katika kazi utakomeshwa.
"Niwambie Tutashughulika na Wazembe hatuko tayari Kuona wananchi wanateseka na uwepo wa watu Wazembe tutashughulika nao"
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amewashukuru Wakazi wa Mwanza kuwa Mstari wa mbele kufata Maagizo yaliyokuwa yanatolewa na serikali kutokana na vurugu zilizojitokeza Oktoba 29 kama vile kukaa ndani wakati wa vurugu.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.