Katika kuhakikisha miradi inatekelezwa kulingana na malengo na viwango vya ubora vilivyowekwa, kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Nyamagana imefanya ziara kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na TASAF.
Ziara hiyo imefanyika March 19,2025 ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi ambaye ni mwenyekiti wa Kamati hiyo na kuwataka wasimamizi wa miradi ngazi zote kuwa wazalendo na kuhakikisha miradi wanayoisimamia inaleta tija katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Kamati imekagua miradi 13 ya Elimu na Afya katika kata tano yenye thamani ya kiasi cha Shilingi 2,455,803,035.25 na kuridhishwa na mwenendo wa utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa namna anavyosimamia na kuhakikisha miradi inaleta tija katika jamii.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la Utawala (122,513,515.00), Bwalo (171,716,392.85),Bweni (175,116,662.84) Shule ya Sekondari Nyamagana- Butimba, Ujenzi wa mabweni mawili Shule ya Sekondari Mahina(355,237,120.00), Jengo la OPD (183,562,392.00), Jengo la upasuaji (148,551,857.00) Zahanati ya Mahina, Ujenzi wa Barabara ya mawe yenye urefu wa mita 426 (249,229,545.45) kata ya Mhandu, Ujenzi wa mabweni mawili (335,072,880.00),Bwalo (147,853,599.00),Vyumba vitatu vya madarasa,Ofisi,matundu 6 ya vyoo (114,167,250.00) Shule ya Sekondari Shamaliwa – Igoma na Ujenzi wa Jengo la IPD (156,008,731.16), Jengo la upasuaji ( 129,116,492.85 na Jengo la OPD (167,656,797.10) Zahanati ya Fumagila - Kishiri.
Aidha mwenyekiti wa Kamati kwa niaba ya Kamati nzima ya Ulinzi na Usalama amewapongeza na kuwashukuru wanakamati wanaosimamia miradi katika kata zote na kuwataka kutokata tamaa badala yake watimize wajibu na kuhakikisha miradi yote inakamilika na kuanza kutoa huduma kwa wakati.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.