Baraza la madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mwanza limepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Uongozi wa hifadhi ya Kisiwa cha Saa Nane ikiwemo kuboresha miundo mbinu na tafiti zitakazowezesha kuongezeka kwa wanyama na kuvutia zaidi watalii wa ndani ambao wanaongezeka kwa kasi kubwa .
Pongezi hizo zimetolewa mapema leo wakati wa ziara ambayo imefanywa katika kisiwa hicho kwa lengo la kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali ikiwa ni sehemu ya majukumu yao kuisimamia Halmashauri Kisiwa cha saa nane kikiwa ni sehemu ya Halmashauri.
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Kisiwa cha saa nane ameshukuru kwa kutembelewa na kuomba asaidiwe kutatuliwa changamoto wanazokumbana nazo kama Hifadhi ikiwepo uvuvi haramu ambao unahatarisha maisha ya viumbe hai waliopo majini na usalama wa maji pia amesema kuwa ghuba ya saanane ndipo mazalia ya samaki aina ya Sato yanapatikana
Akiongea kwa upande wa Halmashauri Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji na Mwakilishi wa Mstahiki Meya ameahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa Hifadhi katika kuzitatua changamoto zinazoikabili hifadhi.
Hifadhi ya Kisiwa cha saa nane inapatikana katika Ziwa Victoria na inapakana na kuzungukwa na kata ya Nyamagana, Pamba, Igogo, Mkuyuni, Nyegezi, Luchelele, Butimba, Mkolani kwa Jiji la Mwanza na Nyamatongo Wilaya ya Sengerema
Wakati wa ziara pia iliwakutanisha Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Mburahati Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam ambayo aliambatana na mwenzake raia wa Kichina ambao baadae walipata fursa ya kuzungumza na wah. Madiwani na kuelezea dhamira yao ya kuwekeza Jijini Mwanza upande wa Uvuvi
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.