Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe.Sima Costantine Sima amefungua Kikao cha wadau wa maendeleo katika ukumbi wa MITU - NIMR kujadili utekelezaji wa mpango kabambe (Master Plan) wa Jiji la Mwanza uliyolenga kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na Kisiasa katika Jiji la Mwanza.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye ni mgeni rasmi katika mkutano huu ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ameanzisha na kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, ujenzi wa soko la kisasa na ujenzi wa stendi ya mabasi ya Nyegezi ambayo tayari imekwishaanza kufanya kazi.
Mhe.Sima amesema kikao hiki kimewezeshwa na Mradi wa Green Cities (SASA Project) kupitia kipengele cha mapitio ya utekelezaji wa Mpango Kabambe huu. Ambapo mradi huu umelenga kusaidia uwekezaji wa miundombinu na ukuaji wa uchumi wa ndani na maendeleo kwa ujumla.
"Mpango huu Kabambe ulizinduliwa mwaka 2019 kama dira ya miaka 20 ambayo ilikuwa ni Mwaka 2015-2035 yakusimamia maendeleo ya Jiji la Mwanza, huku ukitoa mwongozo kuhusu matumizi ya aridhi, mindombinu, mawasiliano na uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa Jiji, ameongeza Mhe.Sima
Vilevile lengo la mpango huu kabambe ni kuboresha huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, ujenzi wa Bandari, upanuzi wa uwanja wa Ndege, uendelezaji wa makazi yasiyo rasimi na uboreshaji wa pwani za ziwa Victoria ili kuvutia watalii na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Hivyo Mhe.Sima amefafanua kuwa kikao hicho kimelenga kufanya mapitio ya mpango huu ili kufanya tathimini ya kuboresha na kuendeleza usimamizi wa utekelezaji wa mpango kabambe huku akiwataka wadau kutoa maoni yenye tija na manufaa yatakayo wezesha kuutekeleza mpango kabambe.
Amemaliza kwa kuwahakikishia wadau kuwa Serikali imejipanga kuendelea kusimamia na kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo itashabihiana na Mpango Kabambe ili kuweza kutimiza ndoto yetu ya kulifanya Jiji la Mwanza kuwa bora na stahimilivu.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.