UZINDUZI WA CHANJO YA POLIO HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA
MKUU wa Wilaya ya Nyamagana Mhe, Amina Makilagi ameongoza uzinduzi wa Kampeni ya Chanjo ya polio na amewasihi wazazi walio na watoto wa chini ya Umri wa miaka mitano (0-5) kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo ya matone ya Polio ili kuwaepusha na ugonjwa huo hatari ambao tayari umeishaingia nchi jirani ya Malawi.
Mhe, Makilagi ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua Chanjo ya Matone ya Polio kwa watoto walio chini ya Miaka (0-5) Katika Zahanati ya Mkolani Jijini hapa ambapo pia ameshiriki zoezi la kuwachanja baadhi ya watoto.
“Kumekuwepo na kasumba ya watu wasiowatakiwa mema kwa kuwatisha kuwa chanjo hizi ni hatari kwa watoto jambo ambalo si kweli bali chanjo hizi ni muhimu kwani mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwa maisha yake na Jamii inayomzunguka na anaweza kuambukizwa magonjwa na kuambukiza wengine pia,” Amesema Makilagi.
Aidha Mhe, Amina ameeleza kuwa kwa sasa wilaya ya Nyamagana imejiandaa kuchanja watoto zaidi ya 92,000, huku chanjo hii ikitolewa majumbani, masokoni,standi,nyumba za Ibada na vituo vya mabasi na sehemu yenye mikusanyiko.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.