Zoezi la kuwapanga machinga lafikia hatua nzuri jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la mwanza ameeleza kuwa zoezi la kuwapanga wafanya biashara wndogo ndogo (machinga) linaendelea vizuri na kwa ufasaha ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wafanya biashara hao wanapata maeneo rafiki kwa biashara zao.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi, mwenyekiti wa kamati ya upangaji wa wafanya biashara hao Desderius Pole jana jumatatu tarehe 11 oktoba 2021 katika soko la mchafukuoga amesema
“Tulianza kwa kuyatambua maeneo na kuwatambua wafanya biashara wadogo wote waliopo katika jiji letu la mwanza tukishirikiana na uongozi wa machinga mkoa na wilaya. Katika kuwapanga wafanya biashara ndogo tulianza na soko lambugani, milongo na sasa tupo katika soko la mchafukuoga. Tumeboresha miundo mbinu kama vile mifereji ili kuepusha athari zitokanazo na maji pamoja na kusawazisha eneo la soko lakini pia tunavyo vyoo vya kisasa katika soko hili. Kwa sasa zoezi limefikia asilimia sabini na kueleza kuwa kufikia tarehe 15 oktoba mwaka huu zoezi litakua limekamilika”.
Kwa upande wao wafanya biashara ndogo ndogo wameeleza furaha yao juu ya jitihada za kuwapanga kuwa haki imetendeka na zoezi linaendelea kwa amani na usalama,
“zoezi limeenda vizuri, utaratibu uliotumika ulikua mzuri, haki imetendeka maana ulikua unaitwa majina yako unapewa namba namba na unahakikiwa kisha unatafuta namba yako kwenye eneo baada ya kuipata linakua eneo lako la biashara”. Hammad Athuman
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.