Mkuu Wa Wilaya ya Nyamagana mhe, Amina Nassor Makilagi kuelekea Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo huadhimiswa kila mwaka 8, March kwa kushirikiana na madiwani, kamati ya ulinzi na usalama, taasisi na mashirika mbalimbali na wanawake kutoka vikundi mbalimbali wameshiriki katika upandaji miti zaidi ya 1800 iliyopandwa katika shule ya msingi kishiri, Kanenwa na shule ya sekondari Fumagira na hii ni kwa sababu kishiri inawatu wengi hivyo itasaidia kupunguza hewa ya ukaa ambayo siyo rafiki kwa afya zetu.
Kutokana na watu kuwa wengi kishiri Mkuu Wa Wilaya amewaagiza mratibu na timu yake kuhakikisha wanasimamia vyema miti iliyopandwa ikuwe vizuri kwa manufaa yetu na kizazi kijacho kwa kuwa TFS wamekuwa wakijitoa kutupatia miti kutoka kwenye vitaru vyao wanavyotumia gharama kuviotesha na hivyo itakuwa vyema tukiwafurahisha kwa kuitunza.
Naye Diwani Viti maalum wa kata ya kishiri mhe, Magreti Paul ameahidi kutunza miti hiyo hata kipindi ambapo kutakuwa hamna nvua, tutajitahidi kumwagilizia ili miti ikuwe tupunguze hewa ukaa ambayo ni hatarishi kwenye mazingira yetu.
Vilevile katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kutambua umuhimu wa watoto wa kike wamepatiwa taulo za kike kwa ajili ya kujihifadhi na kumpatia mwalimu mlezi aweze kuwapatia pindi wakipata changamoto wakiwa katika mazingira ya shule.
Pia kwa upande wa Lwanhima Mkuu wa Wilaya ameshiriki kupanda miti zaidi ya 500 katika shule ya sekunari Sahwa na kuwataka wanafunzi kuitunza ili kuwa na mazingira rafiki ya kujisomea na kula matunda ili kuongeza uwezo wa kufikiri, na amewataka wanafunzi kila mmoja kujichagulia mti wa kuutunza hadi ukue ili kutunza mazingira yetu.
Aidha kikundi cha wanawake kilijitolea kuwapatia wanafunzi taulo za kike kwa ajili ya kujihifadhi kipandi wapatapo changamoto ya hedhi wakiwa shule na mwalimu mlezi alikabidhiwa box 2 kwa ajili ya matumizi ya watoto wa kike.
Mwisho Mkuu wa wilaya amewataka watoto wote kuhakikisha wanamiliki mti mmoja kwa kila mmoja na kuutunza hadi pindi pale anamaliza shule, nakuwahimiza wazazi wao pia kupanda miti nyumbani kwa lengo la kupunguza hewa ya ukaa ambayo ni hatari katika mazingira yetu.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.