Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi, leo tarehe 24 Novemba 2025, ameendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata za Buhongwa na Kishili, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha utawala bora na kutoa huduma kwa ukaribu.
Katika mkutano huo, wananchi wa maeneo hayo wameeleza wasiwasi wao juu ya maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika tarehe 9 Desemba 2025, wakisema matukio ya vurugu yaliyotokea hivi karibuni yamesababisha madhara ikiwemo uharibifu wa miundombinu na kukatiza shughuli za wananchi.
Akizungumza na wakazi wa kata hizo, Mkuu wa Wilaya Mhe. Makilagi amewahakikishia kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama imeimarisha mikakati ya kurejesha na kudumisha hali ya usalama, na kuwataka wananchi kuendelea kulinda amani, kushirikiana na vyombo vya usalama, pamoja na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa sheria.
Ziara hii ni mwendelezo wa jitihada za Serikali ya Wilaya ya Nyamagana katika kusikiliza, kutatua kero na kusimamia usalama wa wananchi wake kwa ukaribu zaidi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.