Wananchi wa Jimbo la Nyamagana wameshiriki vema zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa unaoendelea kote Nchini leo Novemba 27,2024 katika vituo vilivyoandaliwa kwa ajili ya kupiga kura.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Wakili, Kiomoni Kibamba ambaye ni msimamizi mkuu wa uchaguzi Jimbo la Nyamagana ameeleza kuwa wananchi wanajitokeza kwa wingi kupiga kura kwakuwa ni haki yao kikatiba na uchaguzi unafanyika kwa amani nausalamaa.
Mkurugenzi Kibamba ametoa idadi ya waliyojiandikisha ni watu laki nne na elfu sita (406000) huku vituo 1000 vilitumika katika Mitaa 175 na vyama vilivyogombea ni 16 na vyote vilikuwa na mawakala na kufanya zoezi la uchaguzi kuwa vizuri.
Awali vyama vya upinzani vilivyokuwa vinataka kuwasimamisha wagombea wao kama mawakala ikiwa haikubaliki ni kinyume cha sheria na kanuni no 35(6) ya kanuni za Serikali za Mitaa ya Kanuni no 577 ya mwaka 2024 hivyo walileta watu wengine mbadala wakaapiswa na uchaguzi ukaendelea .
Vilevile Ameeleza kuwa waliyodhani kuna vituo vya ziada havipo bali uchaguzi wa mwaka huu unafanywa kwa falsafa ya R4 za Mhe, Dkt.Samia Suluhu Hasan ambazo alitoa kwa viongozi namna ya kuongoza, kuwasikiliza na kuwahudumia.
Kwa upande wake Shekhe Haji Othmani Masasi Katibu wa Baraza la Waislam Mkoa wa Mwanza, amekili kuwa wananchi walikuwa na mwitikio chanya wa kupiga kura nakuwaomba ambao hawajapiga waende wakapige na ambao wamemaliza kupiga waende nyumbani wakatulie wasubili matokeo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.