Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Ndugu Zebedayo Athuman imekamilisha ziara iliyoanza tarehe 16/05/2018-18/05/2018 kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kama inaendana na utekelezaji wa Ilani wa Chama cha Mapinduzi
Kamati imepitia miradi 74 ambayo imegarimu kiasi cha Tsh 4,296,085.00 Miradi iliyopitiwa ni pamoja na Ujenzi wa mradi wa Maji Lwanhima ,Ujenzi wa machinjio ya kisasa Mhandu, ,Ujenzi wa Madarasa Nyashana,Olenjolaay Sekondari,Nyasubi Shule ya Msingi BuhongwaB ,Bugarika Sekondari, Nyakabungo Shule ya Msingi,Nyegezi Sekondari,Kileleni Shule ya msingi, Fumagila Sekondari, Buhongwa Sekondari,Nyakato B,Nyangulugulu, Capripoint Sekondari, Igoma C Mradi wa Umeme wa Jua Shule ya Sekondari Mkolani, Ujenzi wa Matundu ya Vyoo, Shule ya Msingi Kishili na Shule ya Sekondari Mahina,Ujenzi wa Uzio wa shule Shule ya Msingi Nyegezi na shule ya Msingi Mkuyuni, Ujenzi wa zahanati ya Isebanda, Zahanati ya Nyamagana na hali ya Uwanja wa mpira nyamagana.
Wakifanya majumuisho ya ziara hiyo kamati ya siasa ya wilaya imesema imeridhika na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi na kiwango kikubwa unaofanywa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Kamati ya siasa imejiridhisha kwa namna madarasa yanavyojengwa kisasa yakiwekewa marumaru pamoja na dari(gypsum) na kupakwa rangi.Madarasa haya yamejengwa zaidi ya 60 kwa mwaka wa fedha 2017/2018.Hali hii inatia shauku kubwa na Hamasa kubwa kwa Halmashauri zingine kuja kujifunza.
“Tumezunguka tumejionea na kuridhika kuwa tukiendelea hivi tutaishauri serikali wasimtoe hapa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Marry Tesha na Mkurugenzi wa Jiji Ndugu Kiomoni Kibamba wanatekeleza ilani kweli kweli nikiwaangalia naona wanamaono makubwa na wilaya yetu” amesema Ndugu Zebedayo Atuman
Aidha Kamati hiyo imemuomba Mkurugenzi na watalaamu wake wa Jiji kuhakikisha wanafuatilia watalaam wa kwenye kata kwa ukaribu ambapo ndipo hela nyingi za maendeleo hupelekwa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya wananchi.
Akizungumza kwa ajili ya kuiaga kamati ya siasa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndugu Kiomoni Kibamba amesema kuwa kazi yake kubwa ni kuhakikisha antekeleza Ilani ya Chama cha mapinduzi kwa kuwaletea wananchi maendeleo
“Nataka ni hakikishe kufikia 2020, wagombea wa Chama Tawala wanatembea kifua mbele kwa kusema tulikuwa na Vituo vya Afya Vitatu sasa tunavyo vinane, tulikuwa na shule kadhaa sasa tunazo hizi…” amesema Mkurugenzi
Kwa kumalizia Mkurugenzi ameiomba kamati ya siasa kufika mara kwa mara Halmashauri na Kumshauri kila waonapo inafaa na yeye yupo tayari kwa ajili ya utekelezaji.
Muonekano wa Tenki la maji linalojengwa Lwanhima ambapo likikamilika litakuwa na ujazo wa lita 450,000 za maji
Katika picha ni Madarasa Matatu yakiwa yamekamilika kwa kuwekewa chini marumaru najuu dari (gypsum) shule ya sekondari Fumagila
Muonekano wa nje wa Zahanati ya Isebanda ambayo mpaka sasa imekamilika kwa asilimia 98
muonekano wa ndani wa zahanati ya Isebanda
Muonekano wa baadhi ya madarasa yaliyojengwa kwa fedha za P4R na Fedha kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza Shule ya Msingi Nyashana
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ndugu Zebedayo Athuman akimpongeza Mtendaji wa kata ya mbugani kusimamia vyema ujenzi wa madarasa manne shule ya msingi
Nyashana.(Ndani ya Darasa miongoni mwa madarasa manne)
Fundi akiwa katika hatua za mwisho wa ukamilishaji wa Ofisi ya walimu Shule Msingi Azimio iliyopo kata ya Igogo
Muonekano wa nje wa machinjio ya kisasa Mhandu ambapo ikikamilika inatarajiwa kuingiza mapato makubwa kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Mtambo mkubwa wa kuzalisha gesi kutokana na kinyesi cha mifugo umejengwa eneo la machinjio ya kisasa Mhandu
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika hatua ya Msingi ukiendelea Shule ya Msingi Igoma C
Matundu ya vyoo kumi na moja (11) vilivyojengwa shule ya msingi Kishili
Kamati ya siasa ya wilaya ikijirisha kwa kukagua madawati yaliyotengenezwa na shule ya sekondari ya Lwanhima
Mafundi wakiendelea na kazi ya upauaji wa madarasa yaliyojengwa shule ya msingi Buhongwa B
Kamati ya siasa ya wilaya ya Nyamagana wakiangalia uimara wa Dawati lilotengenezwa shule ya sekondari Buhongwa
Umeme wa jua ukiwa umefungwa Shule ya sekondari Mkolani kwa ufadhili kutoka Jiji rafiki la Wuzurburg Nchini Ujerumani
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.