Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameitaka wizara ya mifugo na uvuvi kushirikiana na sekretarieti za Mikoa na za Halimashauri mbalimbali nchini kudhibiti na kutokomeza suala la uvuvi haramu huku akitoa wito kwa wizara na watendaji husika kuwachukulia hatua kali za kisheria wavuvi wote wanaojihusisha na uvuvi haramu.
Dkt.Samia ameyasema hayo Jan 30,2024 wakati wa hafla ya uzinduzi na ugawaji wa boti za kisasa 160 na vizimba 222 vya kufugia samaki kwa wavuvi wa kanda ya ziwa nchini Tanzania ambapo shughuli hii mahususi imefanyika katika maeneo ya kando ya ziwa Kamanga na kukamilisha zoezi hilo katika uwanja wa nyamagana Jijini mwanza ; Zoezi hili limebeba kauli mbiu ‘Uchumi wa bluu ni fursa muhimu kwa wananchi’
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Hamis Ulega amesema kuwa bado yapo mahitaji makubwa kwa watanzania hasa katika suala la vifaa vya kisasa vya kuendeshea shughuli za uvuvi Hivyo pamoja na boti 160 zilizotolewa leo bado tunahitaji boti zisizopungua 500 ili ziweze kuwafikia wavuvi wengine zaidi nchini.
Aidha ameeleza kuwa Boti, Vizimba na vifaranga vilivyotolewa leo vimekatiwa Bima na kwa mkakati uliopo shughuli hii itasimamiwa vyema na sekta ya uvuvi iweze kuongeza pato la Taifa toka asilimia 1.8 hadi asilimia 10kufikia mwaka 2036 hadi 2037 na kuongeza uzalishaji wa samaki kutoka tani laki 5 hadi 7.
Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani amewataka wanufaika wote waende wakafanye vema wavitumie vifaa hivi kuzalisha ”wito wangu kwa wanufaika kwenda kuzitunza Boti hizi, kutumia vyema vifaa hivi vilivyotolewa ili kukuza tija katika sekta hii.” Aidha, amewasihi Wanufaika wasiende kugombana na kuzitaka Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri kusaidia vikundi hivyo ili viweze kufanya vema.
Dkt Samia amewataka wavuvi wote kuzingatia sheria na taratibu za uvuvi na kujiepusha na uvuvi haramu “ suala la kuchoma nyavu kwa lengo la kukabiliana na uvuvi haramu linarudisha nyuma maendeleo ya uvuvi na linagombanisha wavuvi na serikali ; utoaji wa vifaa vya kisasa utaondoa matumizi ya makokolo na hivyo niwaombe Wizara husika muongeze kasi ya utoaji wa nyavu za kisasa kwa njia ya mikopo isiyo na riba ili wavuvi wasitumie nyavu zinazo katazwa.” Amesema Rais Samia.
Sambamba na hilo Rais Samia amesema elimu itolewe kwa wavuvi kwa kuwaeleza madhara ya kutumia makokolo kwamba yanamaliza rasilimali ya mazao ya Samaki.
Mhe. Dkt Samia amezungumza mambo muhimu matatu ambayo ni kuhakikisha uwanja wa ndege wa Mwanza unatumika kusafirisha mazao ya Samaki ikiwa ni Pamoja na kukamilisha ujenzi wa cold room, kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa viwanda vya kusindika mazao ya uvuvi na viwanda vingine na kwamba soko la mazao ya uvuvi liko kubwa duniani na hivyo wanaohusika na uvuvi wafanye kazi sana kwa kuzingatia kanuni zote za uzalishaji, usafi na uchakataji wa mazao hayo ili Tanzania iweze kusafirisha mazao hayo Zaidi.
Akihitimisha hafla hiyo Mhe, Rais ameelekeza Wizara ya Mifugo na uvuvi kufuatilia kwa karibu Zaidi maendeleo ya walionufaika na vifaa vilivyo gawiwa na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa kuwataka wasipunguze lolote katika mizunguko mitatu ya awali ili wawe na ubora katika uzalishaji na uchakataji wa mazao ya uvuvi.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.