Mheshimiwa Waziri wa Afya Jinsia na watoto Ummy Mwalimu amezindua mradi wa Kupunguza vifo vya mama na mtoto ujulikanao kama “ Impact” Jijini Mwanza .Mradi huo umelenga kutekelezwa kwenye wilaya zote Nane zilizoko Mkoani Mwanza na utagharimu bilioni 26 za kitanzania.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mradi huo Mheshimiwa Ummy Mwalimu,amesema serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli imefanya juhudi kubwa ya kuimarisha huduma za afya mijini na vijijini kwa kujenga Zahanati,Vituo vya Afya ,Hospitali za wilaya na kutoa vitendea kazi pamoja na vifaa tiba na utoaji wa ruzuku za dawa.
Mheshimiwa Mwalimu ameendelea kwa kusema “ 2015 Mkoa wa Mwanza ulikuwa na vituo vya afya 5 vyenye nyota lakini kwa sasa Mwanza ina vituo vya afya 117 vyote vina nyota, Mwanza imeendelea kufanya vizuri katika kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 15, mwaka 2015 mpaka asilimia 8,mwaka wa 2018.”
Pamoja na Jitihada zote hizo lakini pia Serikali inasaidiana na wadau mbalimbali kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa “Kwa niaba ya serikali niishukuru sana serikali ya Canada kwa kuchangia sana katika Mradi wa kuimarisha afya ya mama na Mtoto Tanzania”Mhe. Ummy.
Hata hivyo Mheshimiwa Mwalimu akusita kutoa pongezi kwa Mbunge wa Nyamagana Mheshimiwa Stanslaus mabula kwa kuwa kiongozi ambaye anatambua na kupongeza watendaji wa serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuboresha na kuimarisha afya ya Mtanzania.
amesema anaishukuru sana serikali ya Canada kwa kushirikiana na serikali ya jamuhuri ya Muungano kuhakikisha wanaboresha huduma za afya ya Mama na Mtoto kwa kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.
Akisoma Taarifa ya Mradi kwa mgeni rasmi wakati wa hafla hiyo fupi Meneja wa mradi ndugu Edna Selestine, amesema lengo la mradi ni kuwafikia wanawake 653,499 na watoto 83606 chini ya umri wa mwaka mmoja na wanaume 320918.
Mhe.Marry Tesha (Mkuu wa wilaya ya Nyamagana) akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa uimarishaji
wa afya ya Mama na mtoto.
Mbunge wa Nyamagana Mhe.Stanslaus Mabula Mbunge wa Nyamagana akitoa salamu zake kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa Impact
Mhe.Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Bhiku Kotecha,akitoa salamu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mradi wa IMPACT
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.