• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

"SEKTA YA ELIMU HAITAWEZA KUSONGA MBELE KWA MCHANGO WA KUNDI MOJA " , MMHE. MAKILAGI

Posted on: May 30th, 2025

Katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa walimu waliofanya vizuri kwa mwaka 2024, iliyofanyika Mei 30, 2025 katika uwanja wa Nyamagana, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Nassoro Makilagi, alisisitiza kuwa mafanikio ya sekta ya elimu hayawezi kuletwa na kundi moja pekee. Alitoa wito kwa jamii nzima, hususan wazazi, kushirikiana na walimu katika kuimarisha mazingira ya kujifunzia.

"Mafanikio ya sekta ya elimu hayawezi kuletwa kwa kundi moja hivyo niwatake wazazi kushirikiana na walimu kuendeleza baadhi ya miundombinu ambayo wanakuwa wamekubaliana katika vikao, ili elimu bora iweze kupatikana kwa wanafunzi," alisema Mhe. Makilagi.

Aidha, aliwahimiza walimu kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwani kupitia juhudi zao, taifa hupata wataalamu mbalimbali kama madaktari, wanajeshi, marubani na wengine wengi.

"Walimu endeleeni kupiga kazi maana kupitia nyie tunawapata watu wa kada tofauti. Walimu oyeee!" alisisitiza kwa shangwe"

Mhe. Makilagi aliwapongeza viongozi wa shule na walimu kwa jitihada zao, hususan Afisa Elimu wa Wilaya, Mhe. Ally Mussa Rambwe, kwa mchango wake mkubwa katika kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unabaki juu.

Kwa mwaka 2024, ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba umefikia asilimia 93%, hali inayoifanya Nyamagana kushika nafasi ya pili kimkoa. Alitoa wito wa kurejesha nafasi ya kwanza kupitia mshikamano na juhudi zaidi.

Mthibiti Ubora wa Shule Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Lucy Nyanda, alimpongeza Afisa Elimu kwa kuratibu tukio hilo muhimu la kuwajumuisha walimu na kuongeza mshikamano. Alipendekeza mikutano kama hiyo ifanyike mara kwa mara, hata kila mwisho wa mwezi.

Kwa upande wao, wawakilishi wa Benki ya NMB walieleza namna taasisi yao imekuwa bega kwa bega na walimu kwa miaka mingi, wakiahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja za kifedha na kitaaluma.

Shughuli hiyo pia ilihusisha michezo mbalimbali kwa ajili ya burudani na kujenga afya za walimu, ikiwemo kukimbiza kuku, mpira wa miguu, kuvuta kamba, na mbio za magunia. Tuzo zilitolewa kwa walimu na shule zilizofanya vizuri.

Kwa shule za serikali, waliotajwa ni Butimba A, Butimba B, Sahara, na Buhongwa; huku shule za binafsi zilizoibuka ni Buyegu, Mzigu, na Rehoboth.

Hafla hii imedhihirisha kuwa mshikamano baina ya walimu, viongozi, wazazi na wadau wengine ni chachu ya mafanikio ya elimu. Kwa pamoja, ndoto ya elimu bora na mazingira rafiki ya kujifunzia inawezekana.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

    May 31, 2025
  • "SEKTA YA ELIMU HAITAWEZA KUSONGA MBELE KWA MCHANGO WA KUNDI MOJA " , MMHE. MAKILAGI

    May 30, 2025
  • MCHENGERWA AWATAKA MAAFISA HABARI KUWA WABUNIFU

    May 23, 2025
  • DKT. DUGANGE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 25 WA LVRLAC, AHIMIZA UONGOZI BORA NA ULINZI WA RASILIMALI ZA ZIWA VICTORIA

    May 26, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.