Miradi mikubwa 10 yenye thamani ya 4.7 Bilioni yamgusa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa wilayani Nyamagana .
Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Mwanza katika wilaya ya Nyamagana mwaka 2019 umepitia Miradi ya maendeleo 10 yenye thamani ya Sh. 4,781,017,648.79 ikiwa Miradi tisa imezinduliwa na mmoja uliobakia umewekewa jiwe la Msingi moja.
Kaimu mkuu wa Wilaya ya Sengerema amemkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya Dkt. Philp Nyimbi pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa na taasisi za Kiserekali na viongozi wa Dini. Wamepokea Mwenge huo uliokimbizwa na kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ally na kupitia miradi 10.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni pamoja na Mradi wa wakuwezesha kiuchumi Vikundi vya ujasirimali 257, mradi wa ujenzi wa shule ya Msingi, kiwanda cha kufyatulia matolii, ujenzi wa madarasa, Mradi wa maji, kilimo cha kisasa pia Mwenge wa Uhuru umeweza kuzindua makumbusho maalum ya kumuenzi Hayati Baba wa taifa, Ujenzi wa Zahanati, usafi wa mazingira pamoja na ujenzi wa barabara ambayo miradi yote imepokelewa
Miradi yote iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa jambo ambalo kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg Mzee Mkongea Ali amesema Halmashauri zingine zinapaswa kujifunza kutoka Jiji la Mwanza.
Jiji la Mwanza inakua Halmashauri ya Kwanza kimkoa kwa Mwaka huu miradi take yote 10 kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru 2019
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.