Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndg Charles Kabeho ameipongeza wilaya ya Nyamagana kwa kuwa na miradi mikubwa mizuri na yenye tija kubwa kwa wananchi wa Jiji la Mwanza na watanzania kwa ujumla
Sifa hizo zimetolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa wakati Akiaga viongozi,wataalam na wananchi wa Wilaya ya Nyamagana
Aidha Ndg kabeho amesema licha ya Nyamagana kuwa na miradi mikubwa na mizuri ata wananchi pia walihamasika vya kutosha na kushiriki kwa wingi kwa kila miradi iliyotembelewa na kujitokeza kwa wingi eneo la mkesha.
Akitoa taarifa ya Mwenge wa Uhuru 2018 Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe Dkt Phillis Nyimbi amesema zaidi ya wananchi 900 walijitokeza wakati wa mkesha kupima afya na kwa idadi hiyo ni watu Tisa waliobainika kuwa na Virusi vya Ukimwi na kushauriwa kuanza kliniki ya waathirika wa Virusi vya Ukimwi
Mwenge wa Uhuru 2018 Umetembelea miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni Tatu Halmashauri Ya Jiji la Mwanza ikichangia zaidi Ya Milioni mia tatu, Serikali kuu ikichangia zaidi ya milioni miatisa na mchango wa wananchi na wahisani ukiwa zaidi ya Bilioni moja.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja ujenzi wa Barabara ya mawe Isamilo- Nyashana, utoaji wa mkopo wa Shilingi milioni miambili kwa vikundi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Mradi wa maji taka, Soko la Igogo, Mradi wa umeme wa Jua, Club za wapinga rushwa na Vita dhidi ya madawa ya kulevya, zahanati ya Isebanda na Ufunguzi wa shule ya Msingi Buhongwa.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.