• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

Nyamagana kukamilishiwa miradi ambayo haikukamilika katika awamu iliyopita

Posted on: August 17th, 2018


Serikali ya CCM katika awamu ya tano chini ya uongozi wa Mhe Dkt John Pombe Magufuli, imejidhatiti katika mwaka huu wa fedha  2018/2019  kukamilisha miradi  ya maendeleo katika sekta ya Afya ambayo haikukamilika katika awamu iliyopita ikiwemo miundo mbinu ya majengo pamoja na Vifaa tiba wilayani Nyamagana.


Haya yamebainishwa na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula alipokuwa kwenye ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo  katika Kata tatu Isamiro, Pamba pamoja na Kata ya Mahina. Ambapo katika mwaka huu wa fedha 2018/2019 serikali imetenga shilingi . 261,000,000 kukamilisha ujenzi wa Zahanati katika kata hizi tatu.


Mhe Mabula amepata fursa ya kutembelea Zahanati ya Mahina ambayo imepewa shilingi 87,000,000 kukamilisha Wodi mbili ya Wanaume, Mama na Mtoto pamoja na eneo la kupumzikia, vyumba vinne ikiwa ni Chumba cha kujifungulia, chumba  cha kupumzika  baada ya kujifungua na vyumba vinavyobakia ni kwaajili ya Madaktari na wahudumu wa Afya.


Mhe Mabula kadharika ametembelea Kata ya Pamba ambayo imepatiwa shilingi 67,000,000 kukamilisha ujenzi wa wodi Wanaume, Mama na Mtoto pamoja na Chumba cha kujifungulia na mapumziko baada ya kujifungua katika Zahanati ya Bugarika. Kisha akakamilisha ziara yake leo kwa kukagua Zahanati ya Isamiro iliyopatiwa shilingi 107,000,000 kukamilisha ujenzi wa jengo la Zahanati ya Isamiro ambayo ujenzi wake ulianza toka mwaka 2014.


"Mwaka 2015 niliweka ahadi kwa wananchi kukamilisha miradi yote ambayo haikuwa imekamika katika awamu zilizopita. Ninafarijika kuona mwaka 2018 tunakamilisha viporo vyote vya ujenzi wa Zahanati na Vifaa vyake vyote". Mhe Mabula amesema.


Ziara ya Mbunge kesho itaendelea katika kata ya Mhandu na Mkuyuni

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAKILI KIBAMBA ASISITIZA NIDHAMU ENEO LA KAZI

    May 08, 2025
  • WAWEZESHAJI WATOA MBINU ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA KIINGEREZA KUONGEZA UFAULU NYAMAGANA

    May 05, 2025
  • WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

    March 26, 2025
  • DC NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

    March 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.