Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Marry Tesha Onesmo amefanya kikao na wadau wa elimu tarehe 18Juni 2018 kwa lengo la kuboresha hali ya elimu katika wilaya yake.
Akiongea na wadau hao, Mkuu wa wilaya amewaambia wadau hao kuwa jukumu la kupandisha kiwango cha ufaulu katika wilaya ya Nyamagana ni la serikali kwa ushirikiano mkubwa wa wananchi ambao ni wadau wakubwa wa maendeleo.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amesema lazima tuwe na mikakati ya elimu inayotekelezeka ili kuiweka wilaya ya Nyamagana katika nafasi nzuri kielimu ili iweze kusadifu kauli mbiu ya wilaya ya Nyamagana bila ziro inawezekana
“Ni lazima tutokomeze utoro mashuleni,tusimamie nidhamu ya walimu na wanafunzi hii itabadilisha taswira ya taaluma katika wilaya yetu” amesema Mheshimiwa Tesha.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana amewataka walimu kwa ushirikiano na wadau wa elimu kuandaa na kufanya Mitihani ya mara kwa mara ya kata,Wilaya na pia Mheshimiwa tesha amesisitizauwajibikaji wa walimu kutafuta mbinu za kuwapatia chakula cha mchana ili kuboresha hali ya kujifunzia .
Akitoa taarifa ya hali ya taaluma kwa wilaya ya Nyamagana Afisa taaluma wa Elimu sekondari Ndugu Malima Chisumo amesema matokeo ya ufaulu wa mtihani wa Kujipima wa muhula wa kwanza uliofanyika mwezi Mei 2018 kiwilaya kwa shule za Serikali na shule zisizokuwa za serikali.Matokeo ya ufaulu yanaonesha Shule zisizokuwa za serikali zinaufaulu wa juu ukilinganisha na shule za serikali.
Hata hivyo Ndugu Chisumo amesema ingawa Shule zisizozaserikali zimeongoza kwa ufaulu lakini kama wilaya ufaulu haukufikia wastani wa asilimia 90 uliowekwa kitaifa badala yake umefikia asilimia 78.7 Ndugu Chisumo ameomba shule zisizokuwa za serikali kuwa na ushirikiano na shule za serikali ili kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kupandisha ufaulu wa shule zote kiwilaya.
Wakichangia juu ya changamoto na uboreshaji wa ufaulu,wadau wa elimu wamesema changamoto walizonazo ni pamoja watoto kuchelewa shule kwa sababu ya usafiri, kuporomoka kwa maadili kwa baadhi ya walimu na wanafunzi,kutokuwepo kwa mitihani ya mara kwa mara,baadhi ya walimu kutumia lugha ya Kiswahili kufundishia.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.