Ikiwa ni moja ya hatua kubwa ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha usafi unaendelea kuwa sehemu ya tamaduni za shule na jamii kwa ujumla, Halmashauri ya Jiji la Mwanza imekabidhi vifaa vya usafi wa Mazingira katika Shule ya Msingi Fumagila kata ya Kishiri vilivyototolewa kwa hisani ya Mji wa Wurzburg Ujerumani kupitia uhusiano uliopo na Jiji la Mwanza.
Akikabidhi vifaa hivyo leo February 26,2025, Mratibu wa Miji Dada( Sister Cities) Bw. Billy Albert Brown amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa lengo kukabiliana na changamoto zinazopelekea mabadiliko ya tabianchi kupitia makubaliano mahususi na kwamba Halmashauri ya Jiji la Mwanza linatarajia kupata miradi mbalimbali kama nishati rejevu ambayo ni matumizi ya sola.
Pamoja na kukabidhi vifaa hivyo Bw. Brown amewataka Wanafunzi kuwa mabalozi na kuhakikisha jamii inaelewa uhusiano huo mzuri uliopo kati ya Mji wa Wurzburg na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Fumagila Mwl, Dotto Gibebe ameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuwapatia vifaa vya usafi wa mazingira kutokana na Uhusiano mzuri na Mji wa Wurzburg na kudai vifaa hivyo vitaboresha na kutunza mazingira ya shule hiyo huku akiomba uhusiano huo uwawezeshe kisima cha maji kwa kuwa Maji ni changamoto kubwa shuleni hapo.
Vilevile Afsa Rashidi Sadiki akizungumza kwa niaba ya wanafunzi ameushukuru Uongozi wa Jiji la Mwanza kwa kuwapatia vifaa vya usafi na kuahidi kuvitumia na kuboresha Mazingira ya kujifunzia.
Akihitimisha Bw. Billy Brown amewataka wanafunzi wa Shule hiyo kutunza Mazingira na kuahidi kuwa kuhusu changamoto ya maji uongozi wa Miji yote miwili utakaa uone namna ya kutatua changamoto hiyo.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.