Mradi wa Green and smart Cities- SASA unatarajiwa kuboresha sekta za Uchumi, Maji na Mazingira Kwa wananchi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa utekelezaji wa mradi huo tarehe Feb. 20/2024 katika ukumbi mkubwa wa Jiji la Mwanza, Ndugu Patrick Karangwa kwa niaba ya Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Elikana Balandya amesema kupitia mradi huu wananchi wa Mwanza watapata fursa ya kuboreshewa miundo mbinu ya masoko,miundo mbinu ya Maji safi na pia baadhi ya vijana watapatiwa elimu wezeshi ya biashara na pia kupatiwa mikopo ili kukidhi malengo ya mradi.
Karangwa pia alisema, kupitia mradi huu jamii itafaidika na upangaji mzuri wa miji yetu kulingana na mpango kabambe wa miji (Master Plan) ambao tayari umeanza kufanyiwa kazi miaka ya hivi karibuni. Amesema Mwanza ni kati ya miji inayokuwa Kwa Kasi na ina mzunguko mkubwa kati ya miji mikubwa ya Afrika mashariki na maeneo ya jirani.
Ameshukuru wafadhili (team Europe) Kwa kuona umuhimu wa kuleta mradi huu na kuahidi kutoa ushirikiano Kwa mstakabali wa maendeleo ya Jiji la Mwanza.
Naye mwakilishi wa umojanwa ulaya (European Union-EU) Ndg. Martino Jindi amesema ameomba pande zote mbili za timu ya Ulaya na Tanzania kutoa ushirikiano wakutosha huku akisisltiza pande zote kuona mradi huu ni sehemu ya uwajibikaji na utendaji wa Halmashauri hizi wa kila siku na sio kuuchukulia kama nyongeza au kitu ambacho wafadhili wamekileta kwa matakwa yao.
Wakizungumza Kwa pamoja waheshimiwa Madiwani wa Ilemela na Nyamagana wakiongozwa na wastahiki Meya wamewahakikishia wafadhili kuukubali mradi na pia kuwajibika na kutoa ushirikiano Kwa maendeleo ya Halmashauri zao.
Nao Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili wamesifu jitihada za wafadhili na pia kuomba miradi zaidi kama itapatikana ikiwa ni pamoja na ujenzi wa machinjio na dampo la kisasa Ilemela na pia uboreshaji wa barabara katika miradi inayotekelezwa ili iweze kufikika.
Mradi wa Green and smart Cities- SASA unafadhiliwa na EU, GIZ na wafadhili wengine kutoka ulaya na unalenga kutekelezwa Tanzania Kwa mikoa ya Mwanza, Tanga na Pemba.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.