Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Dkt Phillis Nyimbi awatahadharisha wananchi Juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Dkt Nyimbi amewataka wananchi kufanya usafi na kuepuka kutupa taka hovyo ili kujiepusha na Ugonjwa wa kipindupindu .
Dkt Nyimbi ameyasema hayo leo katika kuhadhimisha siku ya usafi ya kitaifa ambayo ni Jumamosi ya kila Mwezi.
Pamoja na kuwatahadharisha wananchi Dkt .Nyimbi amewataka wafanyabiashara hasa wa kata ya Pamba kutokukwepa kufanya usafi katika maeneo yao ya kufanyia kazi, na kusababisha uchafu kuzagaa hovyo.
Hata hivyo Dkt Nyimbi amesema Jiji la Mwanza ni kitovu cha biashara kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na watu wengi kutoka Uganda, Burundi na Kongo huja kwa wingi kufanyabiashara kwenye Jiji hili . Hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa wageni wanaoingia kutoka hasa Congo, Uganda na Burundi ambapo kutokana na taarifa zilizopo imeripotiwa Ugonjwa wa Ebola ambapo mpaka sasa watu wameshapoteza maisha. Hivyo amewaomba wananchi waonapo wageni kutoka maeneo hayo kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika ili kuweza kufikishwa kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupimwa afya zao.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza James Ling'wa amewapongeza mirongo kwa namna walivyojitokeza kufanya usafi na kuwataka kulifanya zoezi hili kuwa endelevu.
Aidha Ling'wa amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Pamba kuhakikisha anasimamia usafi wa mazingira katika Kata ya Pamba.
Maadhimisho ya siku ya usafi kiwilaya Nyamagana imefanyika leo katika Kata ya Mirongo
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.