Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mheshimiwa Marry Tesha Onesmo amezindua maadhimisho ya wiki mazingira Dunianiani katika wilaya ya nyamagana.Uzinduzi huo umefanyika kwa Mkuu wa wilaya kushiriki kufanya usafi katika mitaa ya kamanga Ferry,Barabara ya posta -Stesheni Kanisa la Anglican na Nyamagana Shule ya Msingi
Akizindua wiki ya mazingira Mhe Tesha amewataka wananchi wa Nyamagana kuyatunza mazingira kwa kufanya usafi na kuhifadhi taka maeneo husika. “ninawaagiza TARURA kuzibua mitaro yote iliyoziba kwa sababu ya taka baada ya hapo kila Afisa Afya wa kata na mitaa atawajibika kuwasimamia wananchi kuyasafisha maeneo yao na kutunza mitaro inayopita maeneo yao’’ amesema Mheshimiwa Tesha.
Aidha Mkuu wa wilaya amewahasa wananchi kutumia nishati mbadala badala ya kutumia mkaa ili kuepuka athari za mazingira “ ni nafuu kutumia gesi ambayo utumika muda mrefu kuliko mkaa unaoisha mapema na wenye athari ya mazingira’’amesema Mhe Tesha
Maadhimisho ya wiki ya mazingira Dunianiani yameaanza leo tarehe 31/05/2018 na yatafikia tamati yake tarehe 05/06/2018 kwa kufanyika Kongamano kubwa katika Ukumbi mkubwa wa Jiji.
Maadhimisho haya yanaambatana na kauli mbiu isemayo“Mkaa ni Gharama Tumia Nishati Mbadala” maudhui ya ujumbe huu kitaifa unalenga kuelimisha na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala kwa wananchi ili kukabiliana na changamoto ya ukataji wa miti nchini. Hivyo ujumbe huu unalenga kuonesha madhara ya matumizi ya mkaa kimazingira, kiuchumi na kiafya kwa jamii
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana akiokota taka eneo la Relini leo alipokuwa anaadhimisha wiki ya mazingira wilayani Nyamgana
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Marry Tesha akitoa maelekezo kwa wafanyabiashara wa samaki eneo la kamanga kusafisha maeneo yao wakati akiwa kwenye
maadhimisho ya wiki ya mazingira Duniani
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe.Marry Tesha akiwa na mfuko maalumu wa kuzolea taka
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.