• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam K. Malima ahimiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuongeza makusanyo ya ndani

Posted on: August 3rd, 2022

“nyamagana ya bil 23” twende na kauli mbiu hii. Halmashauri ya jiji la mwanza ndio baba lao katika mapato kuliko halmashauri yoyote katika mkoa wa mwanza na inaweza kufanya zaidi ya bil 20s, nataka mwakani tuweke malengo ya kukusanya bil 26.” Mhe Malima

Maneno ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam K. Malima wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya ya Nyamagana huku akipongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika ukusanyaji wa mapato ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, Halmashauri ilikusanya kiasi cha Bill 18.3 sawa na asilimia 103 ya makisio huku makisio yakiongezeka kwa mwaka huu wa fedha ambapo halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha Tshs Bil 23 ongezeko la Bilioni zaidi ya 5

“Ni Faraja sana mmejipangia malengo ya Tshs Bil 23 na kwa Nyamagana hata Bil 23 bado ni ndogo sensa itaongea tusijiwejkee malengo madogo wala tusijiumize na hapa nataka mwakani tuweke malengo ya Bil 26 lakini hatuwezi kuifikia bila mikakati ikiwemo kuziba mianya ya upotevu wa mapato” Mhe Malima

Akisisitiza uwezo mkubwa wa Halmashauri kimapato Mkuu wa Mkoa wa Mwanza   Mhe. Malima amesema: -

“Baada ya Dar es salaam ni Mwanza kiukubwa na kiuchumi, siwezi kuletwa Mwanza ikazorota, nitakua sijamtendea haki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Nimekuja kuwahamasisha kila mtu afanye kazi katika nafasi yake twende kama timu na ili kazi yoyote ifanikiwe lazima uwatambuie wale wa chini yako, tuhakikishe sisi sote tunakua ni mkakati wa kufikia Nyamagana ya Tshs. Bil 23, hapa  ni kitovu cha kanda ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na Kitovu cha Uchumi kwa Nchi za  Afrika Mashariki tuwavute wenzetu wakiwemo wafanyabiashara wakubwa kuchagua kuja Mwanza badala ya Dar es salaam”

Katika suala la sensa, Mhe. Malima amesisistiza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Wilaya ya Nyamagana  makadilio ya uwepo wa idadi ya watu laki 5 kwa sasa inaweza isiwe sahihi  sana  kwa wakati huu, Kutokana na Ongezeko kubwa sana la watu na ukuaji wa haraka wa Jiji. Tukifanya sensa hii vizuri itatupa picha halisi ya kujua idadi sahihi ya wakazi wa Mwanza na urahisi wa kuwahudumia wananchi wetu. ndio umuhimu wa zoezi la sensa hii inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022,

“Nyamagana ni kubwa na ina watu wengi sana tusiposimamia zoezi la sensa vizuri tutashindwa kuhudumia wananchi, sisi sote tuwajibike katika kulifanikisha zoezi la sensa.” Mhe Malima

Akitoa shukrani zake Mhe. Malima leo amesama “nimekuja kujitamblisha, nimewiwa, kuhemewa na  mapokezi makubwa mliyonipa na kwa bahati nzuri tumeanzia halmashauri hii yenye mambo mengi makubwa zaidi kiuchumi na kimapato kuliko halmasahuri zote ndani ya Mkoa wa Mwanza.

Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutujalia sote kuwa hapa hapa Nyamagana na ninamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye jamii ya wakuu wa Mikoa 26 katika mapenzi yake akaona nafaa kutumika na ninatamka na kumuahidi kuwa uteuzi huu ni sehemu ya kujituma na kuongeza ufanisi zaidi najituma kuutendea haki uteuzi huu, sisi tumetumwa  kwenda kwa watu kufanya kazi yao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Nassoro Makilagi amempongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Rais kwa mara nyingine na kumuahidi ushirikiano kuhakikisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa.

Akizungumza katika kikao cha ukaribisho, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amemuahidi Mhe. Malima ushirikiano,” Nikuhakikishie tumekusikia na kukuelewa dhamira yako ya kuifanya Mwanza mpya kupitia wilaya ya Nyamagana itatimia, tuko tayari kukuunga mkono kuhakikisha maono yako yanatekelezwa”.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Sima Costantine Sima amempongeza Mhe. Malima na kuahidi kuyachukua yote aliyoyaagiza, huku mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Ndg. Athuman Zebedayo akimpongeza Mhe. Malima kwa hotuba yake iliyogusa ushirikiano na kumhakikishia ushirikiano wa kutosha kama Chama.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO KWA WAOMBAJI AMBAO HAWAJAWASILISHA TAARIFA ZAO KWA AJILI YA MNADA April 30, 2025
  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • TANGAZO LA KUPEWA NA KUINGIZWA KATIKA MFUMO WA TAUSI -UPANGISHAJI WA SOKO KUU MWANZA February 21, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAKILI KIBAMBA ASISITIZA NIDHAMU ENEO LA KAZI

    May 08, 2025
  • WAWEZESHAJI WATOA MBINU ZA UFUNDISHAJI WA SOMO LA KIINGEREZA KUONGEZA UFAULU NYAMAGANA

    May 05, 2025
  • WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA HAKI

    March 26, 2025
  • DC NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

    March 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.