“nyamagana ya bil 23” twende na kauli mbiu hii. Halmashauri ya jiji la mwanza ndio baba lao katika mapato kuliko halmashauri yoyote katika mkoa wa mwanza na inaweza kufanya zaidi ya bil 20s, nataka mwakani tuweke malengo ya kukusanya bil 26.” Mhe Malima
Maneno ya Mhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam K. Malima wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya ya Nyamagana huku akipongeza juhudi zinazofanywa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza katika ukusanyaji wa mapato ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, Halmashauri ilikusanya kiasi cha Bill 18.3 sawa na asilimia 103 ya makisio huku makisio yakiongezeka kwa mwaka huu wa fedha ambapo halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha Tshs Bil 23 ongezeko la Bilioni zaidi ya 5
“Ni Faraja sana mmejipangia malengo ya Tshs Bil 23 na kwa Nyamagana hata Bil 23 bado ni ndogo sensa itaongea tusijiwejkee malengo madogo wala tusijiumize na hapa nataka mwakani tuweke malengo ya Bil 26 lakini hatuwezi kuifikia bila mikakati ikiwemo kuziba mianya ya upotevu wa mapato” Mhe Malima
Akisisitiza uwezo mkubwa wa Halmashauri kimapato Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Malima amesema: -
“Baada ya Dar es salaam ni Mwanza kiukubwa na kiuchumi, siwezi kuletwa Mwanza ikazorota, nitakua sijamtendea haki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Nimekuja kuwahamasisha kila mtu afanye kazi katika nafasi yake twende kama timu na ili kazi yoyote ifanikiwe lazima uwatambuie wale wa chini yako, tuhakikishe sisi sote tunakua ni mkakati wa kufikia Nyamagana ya Tshs. Bil 23, hapa ni kitovu cha kanda ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania na Kitovu cha Uchumi kwa Nchi za Afrika Mashariki tuwavute wenzetu wakiwemo wafanyabiashara wakubwa kuchagua kuja Mwanza badala ya Dar es salaam”
Katika suala la sensa, Mhe. Malima amesisistiza kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Wilaya ya Nyamagana makadilio ya uwepo wa idadi ya watu laki 5 kwa sasa inaweza isiwe sahihi sana kwa wakati huu, Kutokana na Ongezeko kubwa sana la watu na ukuaji wa haraka wa Jiji. Tukifanya sensa hii vizuri itatupa picha halisi ya kujua idadi sahihi ya wakazi wa Mwanza na urahisi wa kuwahudumia wananchi wetu. ndio umuhimu wa zoezi la sensa hii inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022,
“Nyamagana ni kubwa na ina watu wengi sana tusiposimamia zoezi la sensa vizuri tutashindwa kuhudumia wananchi, sisi sote tuwajibike katika kulifanikisha zoezi la sensa.” Mhe Malima
Akitoa shukrani zake Mhe. Malima leo amesama “nimekuja kujitamblisha, nimewiwa, kuhemewa na mapokezi makubwa mliyonipa na kwa bahati nzuri tumeanzia halmashauri hii yenye mambo mengi makubwa zaidi kiuchumi na kimapato kuliko halmasahuri zote ndani ya Mkoa wa Mwanza.
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kutujalia sote kuwa hapa hapa Nyamagana na ninamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenye jamii ya wakuu wa Mikoa 26 katika mapenzi yake akaona nafaa kutumika na ninatamka na kumuahidi kuwa uteuzi huu ni sehemu ya kujituma na kuongeza ufanisi zaidi najituma kuutendea haki uteuzi huu, sisi tumetumwa kwenda kwa watu kufanya kazi yao.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Nassoro Makilagi amempongeza Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Rais kwa mara nyingine na kumuahidi ushirikiano kuhakikisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa.
Akizungumza katika kikao cha ukaribisho, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amemuahidi Mhe. Malima ushirikiano,” Nikuhakikishie tumekusikia na kukuelewa dhamira yako ya kuifanya Mwanza mpya kupitia wilaya ya Nyamagana itatimia, tuko tayari kukuunga mkono kuhakikisha maono yako yanatekelezwa”.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Sima Costantine Sima amempongeza Mhe. Malima na kuahidi kuyachukua yote aliyoyaagiza, huku mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana Ndg. Athuman Zebedayo akimpongeza Mhe. Malima kwa hotuba yake iliyogusa ushirikiano na kumhakikishia ushirikiano wa kutosha kama Chama.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.