Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mohamed Mtanda amefanya mazungumzo na Maafisa usafirishaji maarufu kama (Bodaboda) Mei 13, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Buhongwa ‘B’ akiwaeleza sababu za kuzungumza nao ikiwa ni kutambuana, kuzungumza na kufahamiana na makundi mbalimbali ya wanamwanza na kuwajuza kuwa leo ni siku rasimi kwa ajili ya kuzunguza na waendesha pikipiki.
Kupitia mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa ametambua mchango wa Maafisa usafirishaji hao kama ajira binafsi inayochangia pato la Taifa ambapo amesema Mkoa wa Mwanza tunachangia asilimia 7.1
Mhe.Mtanda amewaeleza kuwa serikali inatambua changamoto zinazowakabili maafisa hao, ikiwa ni pamoja na ugomvi baina ya Maafisa usafirishaji wengine kama waendesha Bajaji na magari, na amewahakikishia yupo tayari kumaliza changamoto hizo ili kila mtu atimize wajibu wake ipasavyo.
Pia amewaeleza kuwa anatambua hali ya usalama wao siyo nzuri hivyo basi ameahidi kuhakikisha usalama unakuwepo wa kutosha ili kuunga mkono Sekta binafsi ikiwa ni pamoja na Maafsa usafirishaji ili kuhakikisha wanachangia pato la Taifa, na kuwaboreshea miundombinu ya barabara huku akiwataka na wao kuwa na vibali vinanyowaruhusu kufanya kazi yao ili kuondoa usumbufu kwa watu wa usalama barabarani.
Vilevile ameongelea suala la amani na usalama wa Mkoa wa Mwanza nakuwataja kuwa wao ni wadau wakubwa hivyo hatotaka kuona au kusikia wakijihusisha na makundi yoyote ya kisiasa na kutumia kundi la vijana hawa kwa manufaa ya chama au mlengo fulani wa kisiasa. “fanyeni kazi kwa uadilifu epukeni mambo yanayoweza kuwaingiza kwenye matatizo na kupelekea kugombana na serikali yenu” amesema Mhe.Mtanda.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa kupitia Maafisa Usafirishaji wa Mkoa (RTO) na Wilaya (DTOs) kufanya vikao mara kwa mara ili kutambua changamoto zao na wanapofanya makosa waadhibiwe kwa mujibu wa sheria za Nchi.
Mwisho amezungumzia umuhimu wa Taasisi ya Bodaboda kuwa na ofisi na kuwaahidi kuwaunganisha Vijana na benki ili wakopeshwe pikipiki kwa riba nafuu. Pia ameongeza kuwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ina takribani Bilioni 1.2 kwa ajili ya Mfuko wa uwezeshaji ambapo kwa Vijana ni 4%, wakinamama 4% na wenyeulemavu 2%, na hivi karibuni dirisha lita funguliwa hivyo viongozi na vijana waliojisajili kwenye sekta hii ya Maafisa usafirishaji mtaweza kunufaika.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.