• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

MKUU WA MKOA MWANZA AMEFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI KATIKA UONGOZI NA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: February 2nd, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amefungua rasmi mafunzo ya awamu ya kwanza kwa Waheshimiwa Madiwani waliochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Ilemela, pamoja na Halmashauri za Wilaya za Magu na Ukerewe.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi, Mhe. Mtanda amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwapatia madiwani maarifa na stadi muhimu zitakazowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, hususan katika maeneo ya uongozi na utawala bora, sheria na taratibu za Serikali za Mitaa, pamoja na uendeshaji sahihi wa vikao na mikutano ya kisheria.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo pia yamejumuisha masuala ya uandaaji wa mipango na bajeti, usimamizi wa watumishi, pamoja na ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Mhe. Mtanda amebainisha kuwa bado kumeendelea kuwepo kwa uelewa usio sahihi kuhusu wajibu wa usimamizi wa miradi ya maendeleo, ambapo baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakiamini jukumu hilo limekuwa la Wakuu wa Mikoa au Wilaya pekee, hali iliyosababisha baadhi ya madiwani kujiona kuwa si wajibu wao kusimamia utekelezaji wa miradi.

Ameweka bayana kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo ya madiwani umekuwa ni msingi wa uaminifu waliokabidhiwa na wananchi, na amewahimiza madiwani kusimamia miradi hiyo kwa karibu, kubaini changamoto mapema, kutoa taarifa pale dosari zinapobainika, na kuhakikisha rasilimali za umma zimetumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, ametoa maelekezo kwa wakufunzi kuhakikisha kuwa mada zinazohusu mahusiano ya kiutendaji kati ya Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa zimeelezwa kwa kina, sambamba na kufafanua mipaka ya majukumu kati ya madiwani na watendaji wa serikali katika ngazi ya kata, ili kuepusha migongano na kuimarisha mshikamano katika utekelezaji wa majukumu.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI amesema kuwa mafunzo hayo yamepangwa kutolewa kwa muda wa siku tatu na yamehusisha mada 11, zikiwemo uongozi na utawala bora, muundo na madaraka ya Serikali za Mitaa, pamoja na taratibu za uendeshaji wa vikao na mikutano ya kisheria.

Ameongeza kuwa mada zinazohusu mipango, bajeti, usimamizi wa miradi na udhibiti wa fedha zimeandaliwa kwa lengo la kuwajengea madiwani uwezo wa kusimamia rasilimali za umma kwa uwajibikaji na ufanisi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtanda ametoa maelekezo kwa Halmashauri ambazo bado hazijafikia kiwango cha matumizi cha asilimia 80 ya mashine za POS, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, kuhakikisha zimekamilisha ununuzi wa mashine hizo ndani ya kipindi cha miezi mitatu na zimewasilisha taarifa ya utekelezaji katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA UCHAGUZI October 19, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA SEMINA JIMBO LA NYAMAGANA October 21, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 29, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 09, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MTANDA AFANYA ZIARA YA MIRADI MWANZA, ASISITIZA KASI NA UWAZI WA UTEKELEZAJI

    February 12, 2026
  • MKUU WA MKOA AIPONGEZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KWA MKAKATI WA KUTOKOMEZA UHABA WA MADAWATI

    February 12, 2026
  • RC MTANDA ASISITIZA UKAMILISHAJI WA SHULE YA AMALI KISHIRI NDANI YA WIKI TATU

    February 12, 2026
  • KATIBU TAWALA NYAMAGANA AWAHIMIZA WADAU WA BIASHARA KUSHIRIKIANA KUKUZA UCHUMI

    February 11, 2026
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.