Mkuruguenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ndugu Kiomoni Kiburwa Kibamba atoa somo la maadili kwa watumishi wa Umma. Somo hilo amelitoa alipofanya Kikao na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza jengo la utawala jana.
“ Kumeanza kuibuka tabia kwa baadhi ya watumishi wa umma kutokuvaa mavazi ya haiba na kusababisha heshima ya Halmashauri yetu kushuka” alisema Kibamba.
Mkurugenzi kutokana na baadhi ya watumishi wa Umma kuendelea kutokuvaa mavazi rasmi yanayotajwa na waraka wa Mavazi kwa watumishi wa Umma wa Mwaka 2007. Hivyo ameona ni vyema kukumbushana ili watumishi waishi kwa kuzingatia maadili na Misingi ya utumishi wa Umma.
Aidha Mkurugenzi ameendelea kusisitiza watumishi kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nidhamu wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku “Ni vyema kuwa na lugha yenye staha mnapowahudumia wananchi na watumishi wenzenu kwa sababu ndio msingi wa ninyi kuwa mahala hapa” alisema ndugu Kibamba
Mkurugenzi ameendelea kusisitiza kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia wazembe wasiotekeleza wajibu wao inavyotakiwa kwa sababu akiendekeza wazembe utekelezaji wa Ilani hautafanikiwa ilivyopangwa.
Kikao hiki alichokifanya na watumishi ni mfululizo wa vikao anavyovifanya Mkurugenzi wa Halmashauri mara kwa mara kwa ajili ya kukumbushana na kujadiliana kuhusiana na masuala mtambuka ya Halmashauri.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.