Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ndg Kiomoni Kibamba Kiburwa amekutana na walimu 450 walioamishiwa shule za Msingi kutoka shule za Sekondari na kutoa ufafanuzi wa madai kadha wa kadha waliyokuwanayo walimu.
Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa “Gandh hall” Akiongea kwenye Kikao hicho Kibamba amewaambia Walimu kuwa kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma na Muongozo wa huduma za walimu uliofanyiwa marekebisho 2016 kifungu cha 55 (Techears service sheme) walimu watakaolipwa fedha kwa ajili ya Usumbufu ni wale tu watakaolazimika kufungasha na kuhama na familia zao kutoka kituo kimoja hadi kingine ambapo Mkurugenzi atatoa Usafiri na kuwalipa asilimia 10 ya mishahara yao.
Aidha Mkurugenzi amewaambia walimu tayari amepokea Milioni 393 za EP4R (Education Payment for Result) na Milioni 79 zitalipwa kwa awamu ya kwanza kwa ajili ya kuwamotisha walimu walioamishwa na zingine zitalipwa kwa kadri zitakavyopokelewa.
Ndugu Kibamba amesisitiza kuwa zoezi hili limefanyika bila ya kumwonea mtu yeyote yule hii ni kutokana na Kamati hii kutoa uhuru wa mwalimu kuchagua shule anayoitaji kuhamia, aidha weledi wakamati yenyewe pamoja na jinsi ilivyoundwa kwa kuhusisha Chama cha walimu,TAHOSA,Utumishi,Wadhibiti Ubora na wawakilishi kutoka Umoja wa walimu wa Shule za Misingi.
Kwa kumalizia Mkurugenzi amewataka walimu wote wanaodai malipo yao ya likizo kuanzia Julai,Mosi,2017 fedha zipo na madai yao yatalipwa “ lengo letu ni kuhakikisha hatuzalishi tena madeni yasiyokuwa yalazima” amesema Ndg Kibamba
Kikao cha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na walimu ni utaratibu wa kawaida wa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Ndugu kiomoni Kibamba kukutana na watumishi wa kada mbali mbali na kusikiliza kero zao
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.