Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ashiriki Mkutano wa Kimataifa Korea Kusini Kujadili Mageuzi ya Kidigitali na Ushirikiano wa Miji Dada (Smart Cities)
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba ameshiriki Mkutano wa Kimataifa uliofanyika nchini Korea Kusini, ulioratibiwa na World Smart Cities Forum (WSCF) kwa ushirikiano na Free Economic Zone (IFEZ) pamoja na Association of Smart Cities and Township Alliance (ASAC). Mkutano huo umevuta washiriki kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na Asia.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujadili mikakati ya kisasa ya kuboresha maendeleo ya mijini kwa njia za kidigitali, hususan matumizi ya AI (Akili Mnemba) katika kuongeza ufanisi wa huduma na mifumo ya mijini.
Aidha, washiriki wamejadili kwa kina namna ambavyo miji ya Afrika Mashariki, ikiwemo ile inayozunguka Bonde la Ziwa Victoria, inaweza kushirikiana na miji ya Asia na Ulaya ili kubuni na kutekeleza miradi ya pamoja ya kuimarisha miji, kuendeleza miji endelevu, na kukuza ubunifu wa kiteknolojia.
Miongoni mwa waliowasilisha mada muhimu ni Jaewon Peter Chun, Rais wa ASAC na mwakilishi wa WSCF, pamoja na Dr. Saranchimeg Batsukh, ambao wamebainisha fursa za ushirikiano na njia mpya za kuendeleza miji bunifu duniani.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.