Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kiburwa Kibamba akutana Walimu wakuu wa shule za Sekondari na Misingi kusisitiza Maagizo na Maelekezo ya Mheshimiwa Rais
Mkurugenzi ameyasema hayo leo katika kikao alichokifanya na Maafisa elimu kata,wakuu wa shule na walimu wakuu Katika Ukumbi Mkubwa wa Jiji. “Ninawaagiza kutotoza ama kupokea michango yoyote kutoka kwa wanafunzi ama wazazi .Mzazi yeyote mwenye hiyari ya kuchangia mchango huo atauleta ofisini kwangu” amesema Kibamba
Mkurugenzi ameendelea kuwasititiza walimu hao kujikita zaidi katika kutoa taaluma nzuri itakayosaidia watoto wa kitanzania “Ninachohitaji ni matokeo mazuri hivyo ninawaomba mjikite zaidi katika suala la ufundishaji na udhibiti wa nidhamu za wanafunzi”
Ndg Kibamba ameendelea kuwataka Maafisa Elimu Kata kuwasimamia ipasavyo walimu na kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ipasavyo “Tunataarifa ya Baadhi ya walimu ambao wanaendeleza migomo baridi na kuongea vitu vya hovyo hovyo ninawatakeni Maafisa elimu kata kuwasimamia walimu hawa bila ya uoga ili kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kikamilifu”
Mwisho Mkurugenzi amewataka walimu wote waliohudhuria mafunzo ya mtaala mpya kutoa semina kwa walimu wenzao ili kuwawezesha kuanza kuutumia katika kufundishia
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.