Imekuwa ni kawaida ya binadamu kutoa wasifu wa mtu pale ambapo mauti imemfika mhusika, ambapo wasifu huo huandaliwa vizuri lakini inakua haina maana tena kwa wakati huo maana unayemzungumzia hayupo tena.
Kwa hisia na maono yangu ninasukumwa kuandika makala fupi kuhusiana na mafanikio thabiti aliyoyafanya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa muda wa miaka miwili tangu ateuliwe mnamo Mwezi wa 06.2016
Kwenye Sekta ya Elimu:
Itakumbukwa kulingana na sera ya elimu bila malipo iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Daktari John pombe Magufuli, watanzania wameitikia wito wa kupeleka watoto wao shule na shule nyingi zikafurika kutokana na wingi wa wanafunzi ambao ni dhahiri shahiri kuwa huko nyuma kuna watoto wengi walikosa fursa ya kwenda shule kutokana na malipo yaliyokuwa yanatozwa. Kama ilivyokua katika maeneo mengine hali hii ilitokea pia kwenye Jiji la Mwanza ambapo shule nyingi zilifurika wanafunzi mfano Buhongwa Sekondari, Buhongwa Shule ya Msingi, Nyashana shule ya Msingi, Mtakuja Shule ya Msingi na Nyegezi Sekondari,
Katika kukabiliana na tatizo la uwingi wa wanafunzi ukilinganisha na miundombinu iiyopo na bila ya kupepesa macho, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza amejenga shule 4 mpya za Msingi ambazo ni Samiha S/M, Uhuru S/M, Mwananchi S/M na Buhongwa B S/M sambamba na utengenezaji wa madawati 13571pamoja na ujenzi wa Madarasa 22 katika shule mbalimbali zilizopo ndani ya Jiji la mwanza kulingana na uhitaji na shule husika.
Aidha Mkurugenzi kwa jitihada zake za kuwafikia walimu na kusikiliza kero zao za hapa na pale zimezaa tija kwa kuongeza ufaulu wa kitaaluma kutoka nafasi ya 3 kimkoa mwaka 2015 na kushika nafasi ya I -2016 na 2017 Kimkoa kwa shule za Msingi.
Elimu Sekondari: Kutokana na Jitihada zinazofanywa na Halmashauri ya jiji la Mwanza.Shule za Sekondari zimeendelea kufanya vizuri katika mitihani ya majaribio na mitihani ya kitaifa.Wilaya ya Nyamagana imeendelea kushika nafasi ya 2 Kimkoa kwa mfululizo wa miaka miwili 2016 na 2017 kwa wastani wa asilimia 79 sambamba na ujenzi wa madarasa 54 toka 2016 -2018 katika na utengenezaji wa madawati na viti 41,407 shule za Sekondari
Hata hivyo mkurugenzi amefanikiwa kuleta ulinganifu sawia wa walimu hususani wa masomo ya sanaa kwa shule za Msingi na shule za Sekondari
Sekta ya Mapato:
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukusanya mapato ya Halmashauri licha ya baadhi ya vyanzo vya mapato kuchukuliwa na serikali kuu.
Mkurugenzi amefanikiwa kuibua na kutengeneza vyanzo vya mapato ya Halmashauri kwenye maduka ya Pamba Sekondari, Mwadeko, Sahara na Sweya
Aidha Mkurugenzi ameongeza makusanyo ya Halmashauri kutoka Bilioni 11.7 Mwaka 2015/2016 wakati huo Halmashauri ikiwa inakusanya kodi ya majengo, ardhi na kodi ya mabango mpaka Bilioni 10.5 Mwaka 2017/2018 Halmashauri ikitegemea Leseni ya Biashara, Ushuru wa Huduma
Sekta ya Afya:
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ametekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Kuanza kujenga wadi ya wanaume Hospitali ya Nyamagana, kuimarisha nidhamu ya watumishi katika Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Zahanati ya Kisasa ya Bulale na Isebanda na kuanza ujenzi wa Zahanati ya Nyegezi, Mkuyuni, Isamilo na Mhandu na pia uimarishaji wa Kituo cha Afya cha Igoma.
Sekta ya Maji:
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ameukwamua mradi mkubwa wa maji wa Fumagila wenye tenki la maji lenye ujazo wa Lita 225,000 uliokwama tangu mwaka 2012 ambapo kwa jitihada za Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, mradi wa maji umekamilika na unatumika kwa kuhudumia wananchi zaidi ya 5,100 wa Mtaa wa Fumagila Magharibi na fumagila Mashariki
Aidha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kwa utendaji kazi wa karibu na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh. Stanslaus Mabula wamefanikiwa kutafuta mradi mwingine wa maji unaotekelezwa na wizara ya maji wenye tenki lenye ujazo wa Lita 450,000 unaojengwa kata ya Lwanhima ambao ukikamilika utanufaisha zaidi ya wananchi 12500
Mipango na Uchumi:
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ameandaa miradi mikakati mikubwa na yenye tija ya kuongezea Halmashauri ya jiji la Mwanza mapato, Kuboresha muonekano wa Jiji la Mwanza aidha kuinua uchumi wa wafanyabiashara ndogo ndogo (wachuuzi)
Miradi mikakati hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Soko kuu la Biashara –Kata ya pamba,Ujenzi wa Stendi mpya ya Mabasi –Nyegezi,ujenzi wa stendi ya Malori –Buhongwa,Ujenzi wa Dampo la Kisasa Buhongwa na Ujenzi wa Machinjio ya kisasa Mhandu.
Sekta ya Michezo:
Kwenye mashindano ya UMITASHUNTA,tumekuwa washindi wa Kwanza 2016 na wapili 2017.Hali iliyopelekea vijana 12 kutoka wilaya ya nyamagana kusajiliwa na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu chini ya Miaka 17(Serengeti Boys)
Kwenye mashindano ya UMISSETA,Halmashauri imeendelea kung’ara siku hadi siku kwa kushika nafasi ya kwanza Kimkoa mara tatu mfululizo 2016,2017 na 2018 hali iliyopelekea wachezaji wetu watano kusajililiwa kwenye timu ya Taifa chini ya miaka 19 (Ngorongoro Heroes).
Mafanikio ya Halmashauri ya jiji la Mwanza ni makubwa mno kwa kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya Tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli na Mengi ni ya kuonekana kwa macho na si ya kuadithiwa .
Tutaendelea kutoa makala kuelezea mara kwa mara ili kuleta uelewa wa pamoja wa wananchi, mwisho wa makala hii ni mwanzo wa makala nyingine.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.