• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

Posted on: May 31st, 2025

Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayotarajiwa kufanyika kitaifa tarehe 5 Juni 2025 jijini Dodoma, Wilaya ya Nyamagana leo imefanya zoezi kubwa la usafi wa mazingira katika kata ya Buhongwa, likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi, akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mhe. Makilagi alisema kuwa usafi huo umefanyika kwa pamoja na kata zote za Wilaya ya Nyamagana chini ya usimamizi wa watendaji wa kata na Madiwani na kuongeza kuwa Tanzania inaungana na mataifa yote duniani kuadhimisha siku hii muhimu kwa kutekeleza kaulimbiu ya mwaka huu: "Tanzania Ijayo Tuwajibike Sasa, Dhibiti Matumizi ya Plastiki."

Mhe. Makilagi pia alieleza kuwa Nyamagana ilipangiwa kupanda miti milioni 1.5, na hadi sasa wilaya imevuka lengo hilo hatua inayosaidia kupunguza hewa ukaa na kuchochea mvua.

Aidha, alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 19 Juni 2025 kumpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atakapozindua rasmi mradi mkubwa wa maji kutoka Butimba wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 46.

Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Jiji la Mwanza, Bw. David Joseph, alisema kuwa Siku ya Mazingira huambatana na kampeni za usafi, upandaji miti, na utoaji wa elimu ya mazingira. “Leo tumeungana na wananchi wa Buhongwa kufanya usafi na kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwa vitendo,” alisema.

Vijana nao hawakubaki nyuma. Muajabu Salum, mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Nyaburogoya, kupitia klabu ya mazingira ya shule yao, alieleza kuwa wanaendeleza kampeni ya: “Linda Mazingira, Okoa Maisha”, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Utunzaji wa Mazingira 2022–2032 unaosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mwisho, Mhe. Makilagi aliwahimiza wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1977, na kupuuza kauli potofu zinazodhoofisha ushiriki wa kiraia katika maendeleo ya Taifa.

Matangazo ya Kawaida

  • JITOKEZE KUJIANDIKISHA October 16, 2024
  • TANGAZO LA UPANGISHAJI WA MAENEO YA BIASHARA KATIKA SOKO KUU December 14, 2024
  • UPANGISHAJI WA MAENEO MBALIMBALI YA BIASHARA SOKO KUU May 29, 2025
  • TANGAZO LA MAPENDEKEZO YA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA July 10, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HANANG' WAJIFUNZA MBINU ZA KUONGEZA MAPATO KUTOKA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KUPITIA STENDI KUU YA MABASI NYEGEZI

    June 10, 2025
  • DC AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MIRADI

    June 02, 2025
  • MHE. MAKILAGI AONGOZA ZOEZI LA USAFI BUHONGWA KATIKA UZINDUZI WA WIKI YA MAZINGIRA

    May 31, 2025
  • "SEKTA YA ELIMU HAITAWEZA KUSONGA MBELE KWA MCHANGO WA KUNDI MOJA " , MMHE. MAKILAGI

    May 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

Ziara
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • ESS(Watumishi Portal)
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0755741738

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.