Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe.Sima Constantine Sima aeleza jinsi ushirikiano kati ya Miji na mkakati bora wa kuwezesha utekelezaji wa malengo endelevu katika ngazi za Serikali za Mitaa,
Mhe.Sima aeleza hayo wakati akishirki Mkutano wa Miji Duniani (World Urban Forum) Jijini Cairo Nchini Misri.Mkutano huo umeandaliwa na UN HABITAT kwa ushiriakiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni pamoja na Wizara ya Mazingira ya Finland iliyohusisha Ujumbe wa Jiji la Tampere, Jiji rafiki la Jiji la Mwanza.
Pia ameeleza namna Urafiki wa Tampere na Jiji la Mwanza, umetoa uzoefu wa namna ya kuratibu na kusimamia utekelezaji wa maendeleo endelevu katika ngazi ya Serikali za Mitaa pamoja na namna ya kufanya mapitio ya malengo hayo ili kuendelea kutathimini usimamizi bora.
"Kupitia ushirikiano kati ya Jiji la Mwanza na Tampere, tuliweza kupata maarifa na ujuzi kupitia Jiji la Tampere ambalo tayari lilikwisha zoezi hilo, hivyo kusaidia kufanyika kwa VLR ya kwanza ya SDG katika Jiji letu la Mwanza", amesema Mstahiki Meya Mhe.Sima.
Vilevile, ameeleza kuwa kupitia zoezi hilo la VLR limesaidia kubaini changamoto kwenye sekta mbalimbali ambazo zilipewa vipaumbele na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambapo tayari kuna miradi ambayo imefanyika na mingine inatarajiwa kuanza, ukizingatia miradi ambayo imefanyika ni pamoja na uboreshwaji wa kitengo cha watoto wachanga na Afya ya Mama mjamzito katika Hospitali ya Nyamagana ambao umegharimu kiasi cha shilingi Milioni 180 kwa kununua vifaa Tiba , Vitanda vya joto,kwa watoto na kuboresha Wodi, Mradi utakaotekelezwa na MWAUWASA wa Maji safi na salama na ujenzi wa madarasa katika kuboresha mazingira bora katika kuboresha mazingira ya elimu kwa Wanafunzi.
Mwisho kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ameishukuru Serikali ya Finland, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jiji la Tampere, UN-Habitant Pamoja wadau wote wa maendeleo kwa kuwezesha Jiji la Mwanza kufanya Mapitio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.