Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Wilayani Nyamagana yaonesha muelekeo wa Tanzania ya Viwanda
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanaadhimishwa kila machi 08 ya kila mwaka kwa Wilaya ya Nyamagana maadhimisho haya yamfunguliwa leo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.
Maadhimisho haya uwaleta akina mama sehemu moja na kuonesha jitihada mbalimbali zinazofanywa na akina mama kujikwamua kiuchumi na kijamii.
Katika maadhimisho ya mwaka huu kwa Wilaya ya Nyamagana mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mheshimiwa Mary Tesha Onesmo alipata fursa ya kutembelea mabanda ya wanawake na kujionea shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii zinazofanywa na wanawake.
Shughuli alizoziona mgeni rasmi ni pamoja na utengenezaji wa sabuni za maji na sabuni za miche za kufulia, utengenezaji wa mafuta ya kupaka,utengenezaji Batiki,Vikapu vyandarua pamoja na madawa mbalimbali ya kutibu Binadamu.
Hali hii inaleta faraja na kuakisi kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani nchini "Wanawake kujiwezesha na kujiimarisha na kutafuta usawa kuelekea Uchumi wa Viwanda"
Hali hii inamfanya mgeni rasmi kuona uhalisia wa Tanzania ya viwanda ukitimizwa na wanawake kwa jitihada zao kubwa wanazozifanya hasa wakihamasishana na kuwa vikundi vidogo vidogo vya ujasiriamali vyenye maono ya kufanya vitu vikubwa siku za Usoni
Hali hii inamfanya mgeni rasmi kuwaagiza watalaamu wa masuala mbali mbali waliopo wilayani kuvisaidia vikundi hivi kitaalamu ili kuvisaidia kutimiza dhana ya Tanzania ya viwanda.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.