Katibu tawala Mkoa wa Mwanza afanya ziara ya kikazi Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bwana Ngusa Samike akiambatana na Makatibu Tawala wasaidizi Mkoa wametembelea Halmashauri ya Jiji la Mwanza kukagua miradi Mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Ujenzi wa kituo Cha Afya Bulale, Ujenzi wa Bweni la wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalum Buhongwa Shule ya Msingi,Chanzo cha Maji Butimba na Soko jipya la machinga mchafu kuoga.
Akiwa Kata ya Buhongwa Samike amekagua ujenzi wa Kituo cha Afya Bulale na kuwataka viongozi wa Kituo hicho kuhakikisha eneo lile linaongezwa na kupanga mipangilio ya majengo kabla ya ujenzi ili kuzingatia utunzaji wa mazingira.
"Mpangilio wa majengo kabla ya ujenzi ni muhimu sana siyo unapanda miti leo kutunza mazingira, kabla haijakuwa unang'oa ili kuanza ujenzi.Kituo cha Afya Bulale kimepata Tshs milioni 200 kutoka serikali kuu.
Aidha, amewataka TARURA kuhakikisha ile barabara inayoelekea Kituo cha Afya cha Bulale inatengenezwa ili mazingira yawe rahisi kwa wananchi na wagonjwa wanaofika kituo hicho cha afya.
"TARURA lazima mtofautishe Barabara za kwenye Jiji na za vijijini haiwezekani Jiji ni hapa tuwe na Barabara mbovu kuliko zile za vijijini" Bwana Samike
Baada ya kuondoka Bulale Samike amekagua bweni la wanafunzi wenye ulemavu Shule ya Msingi Buhongwa na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo.
Wakati huo huo, Samike amekagua ujenzi wa mradi wa chanzo cha maji Butimba na kuwataka MWAUWASA kuhakikisha wanawasiliana na Mkoa kila hatua wanapokwama ili kuhakikisha ujenzi unaendelea kwa kazi kubwa.
"Niwatake MWAUWASA wawasiliane na Mkoa ili kuhakikisha ujenzi unaendelea kwa kasi inayotakiwa," alisema Samike.
Katika kuhakikisha wafanyabiashara ndogo ndogo wanafanya biashara zao Kwa amani Bwana Samike amekagua ujenzi wa vibanda vya wamachinga eneo la mchafukoga na kukuta ujenzi unaendelea na biashara zinaendelea.
Hata hivyo, Samike amemalizia ziara yake Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuongea na watumishi wa Halmashauri kwa kuwataka waendelee kuwatumikia wananchi kwa uaminifu mkubwa.
Aidha Bwana Samike amewataka watumishi wote kuzingatia misingi ya maadili ya utumishi wa umma.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.